Denti wa darasa la sita aliyenaswa kwenye kambi ya machangudoa akidaiwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza mwili.Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers imemnasa denti wa darasa la sita anayesoma shule yamsingi (jina linahifadhiwa kimaadili) kwenye kambi ya machangudoa akidaiwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza mwili.
Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita maeneo ya Kahumba mjini Morogoro usiku wa manane ambapo kachero wa OFM alipokea simu kutoka kwa watu walioumizwa na jambo hilo huku wakimwonea huruma kwani alikuwa akichukuliwa na mijibaba.
Mama (Bi. Nasra Hamis) ambaye alikerwa na tabia ya mtoto wa umri huo kujihusisha na biashara haramu ya kujiuza akiwa amesimama karibu naye. OFM ilipofika eneo la tukio ilimshuhudia binti huyo lakini ilipotaka kuita polisi, wenzake waliokuwa wakijiuza naye walikuja juu wakitaka kumshushia kipigo mwanahabari wetu.
Kesho yake OFM ilikwenda kumsaka mtoto huyo ambapo mama aliyejitambulisha kwa jina la Nasra Hamis Ndehere alikuwa miongoni mwa wazazi waliojitokeza baada ya kukerwa na tabia ya mtoto huyo ya kujiuza.
Bi. Nasra Hamis akishiriana na OFM kusaidia zoezi la upatikanaji wa wazazi wa mtoto huyo kwa njia ya simu. Baada ya kumnasa, binti huyo alikiri kujihusisha na biashara hiyo haramu kwa kisingizio cha ukali wa maisha baada ya kufiwa na wazazi wake, alidai alikuwa akitafuta pesa ya kununulia nguo za Sikukuu ya Idd.
...Moja ya wanafunzi wenzake(kulia) aliyedai kuwa amekuwa akitega shule. Pia mtoto huyo alidai kuwa nyumbani kwao ni Mwanza na alipoulizwa kama anaweza kuwasiliana na ndugu zake alijibu anaweza hivyo alipewa simu ili awapigie lakini namba zao hazikuwa hewani.
OFM kwa kushirikiana na mama huyo waliamua kumpeleka mtoto huyo Ustawi wa Jamii.
Umati ukishuhudia mkasa huo wa mwanafunzi wa darasa la sita wakati akihojiwa.
Katika hali ya kushangaza, wakati wanaelekea Ustawi wa Jamii, walikutana na msichana ambaye baada ya kuwaona alisema binti huyo siku hizi haonekani shuleni kwani anasoma naye darasa moja.
Kufuatia kauli hiyo, mama huyo alimshushia kichapo kikali denti huyo hivyo kujaza umati.
1 comment:
Sijui wapi tunakoelekea hivi sasa,kitoto kidogo na bado kuwa tayari kumkabili mwanmaume sijui mtu utapata nini kutoka nacho,hii ni laana inatushukia toka kwa mwenyezi mungu.
Post a Comment