Sunday, 28 December 2014

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KATA ZA MBANJA NA RASIBURA HUKO LINDI MJINI‏


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi wa Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Diwani wa Kata ya Mbanja Ndugu Said Juma Hamid wakati akiwasili kwenye Ofisi ya Tawi la Mbanja kwa ajili ya kikao cha ndani na wajumbe hao tarehe 27.12.2014.


Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa Tawi la CCM la Mbanja. Mama Salma alitembelea tawi hilo tarehe 27.12.2014 kwa ajili ya kukagua kazi ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.

Baadhi ya wajumbe wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Mabano katika Kata ya Mbanja wakifurahia hotuba ya Mjumbe wa NEC Taifa wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete wakati alipotembelea Tawi hilo tarehe 27.12.2014.

Katibu wa Shina la Wakereketwa Zahanati Kempu Ndugu Hidaya Chivi Ali akikabidhi risala ya wanachama wa Shina hilo kwa Mjumbe wa NEC Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 27.12.2014.

Mjumbe wa NEC Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipandisha bendera ya Chama Cha Mapinduzi katika Shina la wakereketwa Zahanati Kempu wakati wa sherehe ya uzinduzi wa shina hilo lililoko katika Kata ya Rasibura huko Lindi Mjini tarehe 27.12.2014.

Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akisoma maelezo yaliyoko kwenye jiwe la msingi la shina la wakereketwa Zahanati Kempu mara baada ya kuzindua rasmi shina hilo tarehe 27.12.2014.


Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na vijana na wananchi mara baada ya kuzindua rasmi shina la wakereketwa Zahanati Kempu lililoko katika Kata ya Rasibura tarehe 27.12.2014.
 

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanachama wa shina la wakereketwa Zahanati Kempu mara baada ya kulizindua rasmi tarehe 27.12.2014.




 Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM Ndugu Nurdin Shaweji aliyejiunga na Chama hicho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tawi la Stendi lililoko katika Kata ya Rasibura tarehe 27.12.2014.

Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Rasibura katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tawi la Stendi huko Lindi Mjini tarehe 27.12.2014.

PICHA NA JOHN  LUKUWI 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!