Monday 22 December 2014

CHANZO NA TIBA YA MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO (U.T.I)

Maambukizi katika njia ya mkojo au katika kibovu cha mkojo, tatizo hili SI miongoni mwa magonjwa ya zinaa (STDs)
Mara nyingi tatizo hili husababishwa na bacteria anajukanae kama E.coli,



JINSI UNAVYOENEA
UTIs ni tatizo miongoni mwa watu hasa wanawake hasa wenye uke kwa sababu ya uwazi wa urethra kuwa karibu sana uke na tundu la haja kubwa.
Kuna bacteria hatari kutoka tumboni na kuingia katika njia ya mkojo urethra kwa kuwafuta au kuwapangusa kutoka kwenye huo uwazi wa uke na tundu la haja kubwa.

Vile vile watu wenye uke (wanawake)  wana mrija mfupi sana wa urethra (mrija wa mkojo) hivyo kwa sababu hiyo ni rahisi kwa bacteria kusafiri na kuingia kwenye kibovu cha mkojo na kusababisha maambukizi.

Kibofu cha mkojo (bladder) ni kiungo ambacho hutunza mkojo kabla ya mkojo kuingizwa kwenye mrija urethra wake ili utoke njekwa njia ya kukojoa.



NINI DALILI ZAKE

Dalili za maambukizi katika njia ya mkojo (UTIs) kama yafuatayo;

Kukojoa mara kwa mara kusiko kawaida;

Maumivu kama ya kuwaka moto wakati wa kukojoa (kama unaunguzwa na mkojo);
 
Mkojo kutoa harufu isiyo ya kawaida;
Mkojo kuwa na hali ya damu ndani yake;

maumivu ya tumbo la chini mara nyingine;
Pia homa.
JINSI UCHUNGUZI UNAVYOFANYIKA.
Mara zingine uchunguzi wa haya Maambukizi katika njia ya Mkojo yana unaweza kufanyika kwa kuchunguza dalili hizo nilizo taja hapo juu.
Vile vile huweza kufanyika kwa kupima Mkojo, mkojo kupelekwa Maabara kwa uchunguzi zaidi ambapo huchunguzwa kwa kupima kuwepo kwa Bacteria wasababishao maambukizi hayo (E.coli)

NINI MATATIZO YAKE.
Endapo kama maambukizi haya ya njia ya mkojo hayatotibiwa mapema na kimamilifu, maambukizi yanaweza kusambaa mpaka kwenye mfumo wa mkojo wa juu (kwenye kibofu na figo kuathirika),

Na inapofikia hali hiyo ya maambukizi basi inaweza kupelekea kulazwa hospitalini.

Pia, maumivu yanapokuwa ya hali ya juu, hasa maumivu ya tumbo la chini, mkojo kuwa na  damu, haraka sana mwone mhudumu wa afya iwezekanavyo.

JINSI INAVYOTIBIWA.
Maambukizi katika njia ya mkojo (UTIs)
Tiba yake ni rahisi tu ambapo ANTIBIOTICS tu hutumika, (ni vizuri dawa hizo majina yake uende moja kwa moja hospital ukaandikiwe na daktari kulingana na kiwango cha maambukizi kilivyo na sababu zingine utakazokuwa nazo ndio maana sijaandika ni aina gani ya ANTIBIOTICS zinazotakiwa).

Ni muhimu sana kumaliza dozi uliyopangiwa hata kama dalili zote zimekwisha ni lazima umalize dozi hiyo.

Kama dalili ulizokuwa nazo hazikuisha mpaka dozi inakwisha basi tambua ya kuwa, kuna uwezekano kuwa bacteria wamekuwa sugu kwenye hiyo aina ya dawa uliyotumia.

Na utashauriwa kuchunguzwa upya na kutibiwa upya.


Habari gani kuhusu Mpenzi wako ama mwenza wako endapo wewe unapata Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTIs)?
Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTIs) sio ugonjwa wa zinaa .
Lakini kujishughulisha na Ngono kunaweza kupelekea maambukizi haya na kumbuka mpenzi au mwenza wako hahitaji kutibiwa.



KUZUIA MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA MKOJO.
Unaweza kuzuia (sio kutibu)
Kwa kufanya yafuatayo;
Kunywa mpaka glass sita za maji kwa siku;

Kunywa kwa wingi juisi chachu ya Cranberry (jamii ya matunda Damu)


Kojoa mara kwa mara kadiri iwezekavyo.
Kojoa kabla na Baada ya tendo la ngono/ndoa

Jipanguse/jisafishe kwa kutoka mbele kwenda nyuma mara baada ya kuoga au baada ya kujisaidia. (namaana wakati wa kuchamba basi ni vyema ukajisafisha kwa kupeleka nyuma na sio mbele upande wa uke ilipo urethra)


Vaa chupi au nguo za ndani zisizo bana sana na hasa si vizuri kuvaa nguo za jamii ya nailoni, ni vizuri kuvaa nguzo za ndani jamii ya pamba ni nzuri zaidi.
Oga Mara kwa Mara

Pia, kama unajua una Maambukizi katika njia ya mkojo basi fanya haya;
Jizuie au acha kunywa chai, kahawa, bia, mvinyo na vitu kama hivyo vyenye jamii ya alkali ndani yake.

Jihadhari na juisi ya machungwa kwa sababu vyote hivyo hubadilika na kuwa alkali ndani ya mwili ambayo huchangia bacteria kukua ndani ya mwili asababishae UTIs.

Tumia vitamin C kama kichochezi asilia cha kufanya ukojoe mara kwa mara.

Kitu kingine cha muhimu cha kuzingatia ni kuzuia kutumia vimiminika/vinywaji.

Makala hii inalenga kukupa mwanga nini juu ya ugonjwa huu wa maambukizi katika njia ya mkojo ili uweze kujua ni namna gani ya kukabiliana nayo.
Endapo hali inakuwa tofauti basi wahi kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.  


KWA HISANI YA NYANDA HEALTH

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!