Wednesday 26 November 2014

WAKE WENYE VVU WAPEWA TALAKA LINDI

Baadhi ya wanaume mkoani hapa wanadaiwa kuwanyanyapaa wake zao kwa kuwapa talaka pindi wanapogundulika wana na maambukizi ya virusi Ukimwi.

Wataalamu wa afya kutoka Zahanati ya Mitwero walisema hayo jana walipokutana na timu ya Shirika la Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation (EGPAF).
Muuguzi Grace John na Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Ally Daudi walisema baadhi ya wanaume hukataa kupima afya zao pale wanapoombwa na wake zao ili waweze kufahamu kama wapo salama au la.
Dk Daudi alisema kutokana na hali hiyo wanawake huchukua uamuzi wa kupima VVU na kama wakigundulika wameathirika, hunyamaza kwa kuhofia kupewa taraka.
“Hivi ninapozungumza na ninyi leo hii kuna mama mmoja alimweleza mumewe wakapime ili kutambua afya zao, mume alimkatalia, lakini mwanamke huyu alipokuja na kubainika ana VVU, tulimuanzishia dawa.
“Lakini akasema atalazimika kuzificha chini ya ndoo ya maji ili asiachwe na mumewe,” alisema Dk Daudi.
Muuguzi John alisema alishawahi kusuluhisha ugomvi wa wanandoa wawili, waliofika kupima afya zao na mwanamke aliyegundulika kuwa na VVU huku mwanamume akiwa hana.
“Baada ya wanandoa hao kufika hapa kupima afya zao, mwanamke alikutwa na maambukizi, lakini mwanamume hakuwanavyo, kulitokea vuta nikuvute, mwanamume alikwenda dukani kununua karatasi na peni kutaka kumwandikia mkewe talaka mbele yangu,” alisema.
Alisema kutokana na jitihada za kusuluhisha ugomvi huo, wanandoa hao walifanikiwa kupatana na kuweza kurejea nyumbani kwao

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!