Monday, 3 November 2014

U T I ISIPOTIBIWA MAPEMA HUCHANGIA KUTOPATA UJAUZITO



Swali : UTI ni nini ?
Dk. Mwaka: UTI ni kifupi cha neno ( Urinary Track Infection) au maambukizi katika njia ya mkojo na bahati nzuri tunapozungumzia njia ya mkojo hatumaanishi kwamba ni sehemu ndogo ya mwisho ya mkojo, bali inabeba sehemu kubwa kuanzia kwenye figo, mirija ya kusafirisha mkojo na kibofu cha mkojo na sehemu ya mwisho ambayo inatumika kutoa mkojo nje.

Swali: Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango, je yanaweza sababisha uvimbe katika mfuko wa uzazi?
Dk. Mwaka: Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango kama zitatumiwa kwa mpangilio mzuri hayana madhara, lakini kutokana na baadhi ya watu kuzitumia vichochoroni na wanawake kuelekezana wenyewe kienyeji pasipo kufanya vipimo, lazima zimletee madhara makubwa mtumiaji. Miongoni mwa madhara hayo ni kuvuruga viwango vya homoni.
Tafiti zinaonyesha kuwa kinachofanya mwanamke kupata uvimbe na ukue ni matumizi mabaya ya vidonge vya uzazi wa mpango ambavyo mwanamke akivitumia sana basi huenda kugeuka vijivimbe katika mfuko wake wa uzazi.
Swali: Kwanini tatizo la kutopata ujauzito limekua kwa kiasi kikubwa hivi sasa?
Dk. Mwaka: Tatizo hili lilikuwepo, lakini kutokana na uwazi wa habari ndio limeonekana kuongezeka kwa kasi. Tukirudi kwa wanawake wa mjini ni kweli tatizo hili linaonekana kuongezea kutokana na sababu mbalimbali kumekuwepo na mambo mengi ambayo yanaweza kusababisha mwanamke kushidwa kupata ujauzito.
Tukianza na tatizo la ukomaaji wa mayai na kama mwanamke mayai yake hayakomai vizuri, hawezi kupata ujauzito na vitu vinavyofanya mayai ya mwanamke kushidwa kukomaa ni vingi sana, mfano kuwa na msongo wa mawazo na kitu kingine kinachofanya wanawake washidwe kupata ujauzito ni kuziba kwa mirija ya uzazi.
Tatizo hili hutokana na magojwa ya ngono au fangasi wa muda mrefu, pia UTI iliyokaa muda mrefu bila kutibiwa. Hivyo, wanawake wanashauriwa kuwa makini na afya zao hasa katika mambo ya uzazi.
Swali: Je tatizo la kuhama hama kwa kizazi linasababishwa na nini ?
Dk. Mwaka: Tatizo la kizazi kuhama au kushuka huwa hakuna sababu za msingi, hii hutokana na maumbile. Pia tatizo hili hutokana na tabia za mwanamke, unakuta kuna baadhi ya wanawake wanatembea kwa kujibinua na hali hiyo inapofanyika kwa muda mrefu, hali inayochangia kuharibu kizazi chake.
Kinajisogeza mbele au kubinuka juu, hii inasababisha mwanamke kushidwa kushika ujauzito kwa sababu pale mbegu zinaporuhusiwa kuingia hazitaweza kupenya kutokana na kizazi kubinuka.
Kwa leo tuishie hapa, ila angalizo kwa mwanamke yoyote ambaye unaona una matatizo katika mfumo wako wa uzazi, jitahidi kuepuka vitu ambavyo vitakulelea matatizo hayo.
Swali: Je, inawezekana mwanamke akawa na uvimbe katika kizazi na akaweza kujifungua salama?
Dk. Mwaka: Kesi kama hizi nyingi hutufikia katika kituo chetu hapa Foreplan Clinic. Kitu cha kwanza tunatakiwa kufahamu kuwa uvimbe unapokuwa mkubwa huchukua sehemu kubwa ya mfuko wa uzazi, hivyo mimba inakuwa ni ngumu kuendea kukua au mimba inaweza kukua, lakini inapozidi kuwa kubwa hulazimika kutoka, ndipo tunaita mimba imeharibika.
Kitu cha pili ni ule uvimbe unaokuwa ndani ya kizazi huweza kunyonya damu yote na wakati huo huo mtoto naye anahitaji damu ya kutosha, hivyo akikosa damu hushindwa kuendelea kukua na hatimaye huharibika.
Kitu kingine ni ule uvimbe unapokuwa umekalia ndani ya kizazi kwa ndani kabisa humzonga mtoto na kusababisha mimba kutoka. Kwa bahati nzuri katika kituo chetu cha Foreplan Clinic, tunapenda mwanamke aje tumsaidie akiwa hajapata ujauzito na ikitokea bahati mbaya uko aliko akapata ujauzito na akawa na uvimbe pia tunachoweza kumsaidia kwa kumpatia dawa ambazo zitamsaidia kuufanya ule uvimbe usinyae, ili mtoto aliyeko tumboni aweze kukua bila kupata madhara yoyote.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!