Monday, 17 November 2014
STARS YATOKA SARE NA SWAZILAND
TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars jana ilitoka sare bao ya 1-1 dhidi ya wenyeji wao Swaziland katika mechi iliyochezwa mjini Mbabane. Mechi hiyo ilikuwa ya kimataifa ya kirafiki inayotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Kabla ya kwenda Mbabane, Stars ikiwa na wachezaji 20 iliweka kambi ya siku tatu Johannesburg, Afrika Kusini. Habari kutoka Mbabane zinasema mchezo ulikuwa mkali, lakini mwamuzi anadaiwa kuiuma Taifa Stars.
“Mchzeo ulikuwa mzuri, huku Swaziland hali ya hewa ilikuwa baridi kali sana, vijana walijitahidi sana, lakini kuna mambo mengine sio ya kulalamikia, waamuzi hawakuchezesha kwa haki hata kidogo, alitunyima penalti ya wazi kabisa na alitoa kadi za njano nyingi upande wetu bila mpangilio,” alisema mshauri wa masuala ya kiufundi wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamali Malinzi, Pelegrinius Rutahyuga.
Rutahyuga alisema bao la Stars lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa anayecheza soka ya kulipwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Thomas Ulimwengu.
Rutahyuga alisema Stars inatarajiwa kurejea nchini leo kujiandaa na ratiba nyingine.
Wachezaji waliokwenda Mbabane chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij ni Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wanaocheza TP Mazembe, Mwinyi Kazimoto anayecheza soka ya kulipwa Qatar na Juma Lazio anayechezea Zesco ya Zambia.
Wengine ni nahodha Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Amri Kiemba, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Deogratius Munishi.
Aidha wengine ni Aishi Manula, Said Moradi, Oscar Joshua, Himid Mao, Emmanuel Simwanda, Salum Abubakari, Saidi Ndemla, Haruna Chanongo, Simon Msuva, Abubakar Mtiro, Hassan Isihaka, Erasto Nyoni na Salim Mbonde.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment