HALI ya Rais Jakaya Kikwete ambaye mwishoni mwa wiki alifanyiwa operesheni ya tezi dume, inaendelea kuimarika na ameanza kufanya mazoezi ya kutembea.
Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Rais Kikwete ameanza kufanya mazoezi ya kutembea siku ya pili tu baada ya kufanyiwa operesheni ya tezi dume kwenye Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Maryland, Marekani.
Aidha, imeahidi kuendelea kuwapatia wananchi habari sahihi kuhusu maendeleo ya afya ya Rais Kikwete kwa kadri habari hizo zitakavyokuwa zinapatikana.
“Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kuwashukuru sana wote ambao wamekuwa wakimwombea Rais Kikwete, ili apone haraka na kurejea nyumbani kujiunga na wananchi wenzake katika ujenzi wa taifa letu. Tunawaomba muendelee kumwombea,” imesema sehemu ya taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana
No comments:
Post a Comment