Tuesday 2 September 2014

WANNE MBARONI KWA MAUAJI KATAVI

index
Na Kibada Kibada –Katavi.
Watu wanne wanashikiliwa na Polisi Mkoani Katavi kwa tuhuma za kuhusishwa na mauaji ya mtoto aitwaye Regina Geofrey mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili,kasha kumzika kwenye kibanda cha Baba wa mtoto aliyeuwawa kinachotumika kufanyia shughuli za uganga wa kienyeji.


Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kuwataja watu wanaotuhumiwa kuwa ni wazazi wa mtoto Regina,ambao ni baba mzazi  wa mtoto aliyefahamika kwa majina manne ya Geofrey Kilangwa( Maarufu kwa jina la  Charles Simbaiwe) miaka (27) na mama mzazi wa mtoto aitwaye Maria Exavery miaka (22) mkazi wote wakazi wa Kitongoji cha Mwikang’ombe kijiji cha Katauma Kata ya Katuma Tarafa ya mwese Wilayani Mpanda.
Kamanda amewataja watuhumiwa wengine kuwa Masolwa Jacob (29) Mkazi wa Mwikang’ombe Kata ya Katuma,na Regina Kaboni miaka (40) Mkazi Isamilo Jijini Mwanza na wote wanashikiliwa kwa mahojiano na jeshi la Polisi watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kwa Mjibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kidavashari alieleza kuwa tukio hilo limetokea mwishoni mwa mwezi Augusti katika kitongoji cha Mwikang’ombe kijiji cha Katuma Kata ya Katuma Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Katika tukio hilo mtoto huyo aliuwawa na kuzikwa katika Kibanda cha kufanyia shughuli za uganga wa kienyeji ambacho ni kibanda cha baba yake  mzazi wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Geofrey Kilangwa maarufu kwa jina la Charles Simbaiwe ambaye ni mganga wa kienyeji.
Akifafanua zaidi Kamanda Kidavashari alieleza kuwa inasemekana kwamba mtoto Regina alikuwa anaumwa ugonjwa ambao ulikuwa haufahamiki kwa takribani mwezi mmoja kitendo kilichopelekea auguzwe kienyeji na baba yake mzazi pasipo kumfahamisha mama yake mzazi alimficha.
Kutokana na kumadanganya mke wake kuwa mtoto alipelekkwa kwenye matibabu kwa babu yake huko mkoani mwanza kumbe alikuwa amekufa na kuzikwa kwa siri.
Kutokana na kutoonekana kwa Mtoto huyo kwa takribani mwezi mmoja wakazi wa kitongoji hicho wakiongozana na mwenyekiti wao walianza kutilia mashaka hali hiyo na kuanza kufuatilia suala hilo kutokana na tetesi zilizokuwa zimezanga katika kitongoji hicho kuwa mtoto aliuwawa na baba yake mzazi na kwa imani za kishirikiana ,shughuli za kiganga hivyo waliamua kufika nyumbani kwa Geofrey Kilangwa kumhoji kuhusiana na suala hilo ambapo alipinga kuhusika na walipopekuwa katika kibanda ambacho hufanyia shughuli zake za tiba walopna kukiwa na tuta dogo lililoonekana kufukiwa na udogo ulioonekana kuchimbwa siku za karibuni na ndipo walipoamua kufukua na walikuta kichwa cha mtoto kasha kutoa taarifa Polisi.
Watuhumiwa wote wanatarajiwa  kufikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokuwa umekamilika.
Katika tukio jingine  huko katika kijiji cha Luchima Kata ya Majimoto Tarafa ya Mamba Wilayani Mlele mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Credo Amando Maarufu kwa jina la Kamyola miaka (58) aliuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na watu waiofahamika.
Kamanda Kidavashari alieleza kuwa tukio hilo lilitokea August 29,mwaka huu majira ya majira ya saa nne asubuhi katika kitongoni cha Kawanga Kijiji cha Luchima.
Siku ya tukio majira ya saa tatu asubuhi marehemu alionekana nyumbani kwake akijiandaa kwenda kwenye shughuli zake za kila siku za uvuvi na ilipofika majira ya saa saba mchana ndipo mwili wa marehemu ulipobainika ukiwa katika ngarawa maeneo ambayo ni pembezoni mwa fukwe za mto Kavuu ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake .
Na katika tukio hilo hakuna mtu aliyeshukiwa kuhusika na tukio hilo na hakuan mtu aliyekamatwa ingawa inadaiwa marehemu alikuwa na tabia ya ulevi uliokithiri,jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kuwasaka wahusika wa tukio hilo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!