Saturday, 13 September 2014

TUNAWEZA KUPUNGUZA KASI YA AJALI

CHAMA cha Kutetea Abiria nchini (Chakua), kimesema kinaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa ajali ndani ya miezi miwili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa chama hicho, Penatus Kapira alisema ajali zinatokana na watendaji kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani.
Alisema utaratibu watakaotumia kutokomeza tatizo hilo ni kuweka maofisa wa chama hicho katika magari ya umma ambao watatoa elimu kwa abiria juu haki na kuwaelimisha sheria za usalama barabarani kisha kuripoti taarifa za dereva atakaevunja sheria.
Hata hivyo, alisema ili mpango huo ufanikiwe chama hicho kinaomba ufadhili na wadau mbalimbali kuwasaidia sh milioni 25 za kuanzia mapambano hayo.
Ofisa wakutetea abiria wa chama hicho, Gervas Rutaguzinda alisema baadhi ya wamiliki vyombo vya usafiri ni chanzo cha ajali hizo kwa kuwa wanawalazimisha madereva kuendesha magari mabovu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!