Saturday, 6 September 2014

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA CHAKULA CHA JIONI CHA KAMPENI ZA KUPAMBANA NA UTUMIKISHWAJI WA WATOTO

IMG_1294 (1)Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiingia kwenye kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena kwa ajili ya chakula cha jioni cha kampeni za kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa nchini kilichoandaliwa na Shirika la International Rescue Committee tarehe 5.9.2014

IMG_1302 (2)Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo.
IMG_1322Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Msanii maarufu wa kimataifa Daniele de Niese anayetumiwa na Shirika la International Rescue Committee katika kuhamasisha mapambano ya utumikishwaji wa watoto.
IMG_1328Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Dkt Augustine Mahiga wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na International Rescue Committee  kwenye hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014 kwa ajili ya kuhamasisha mapambano dhidi ya utumikishwaji wa watoto hapa nchini.
IMG_1339Msanii wa Kimataifa anayetumia kipaji chake cha kuimba Daniele de Niese akiimba nyimbo mbalimbali kwa lugha mbalimbali, kiingereza, kifaransa, kitaliano wakati wa chakula cha jioni katika kuhamasisha mapambano dhidi ya utumikishwaji wa watoto.
IMG_1352Mtoto Hamadi Hatibu, 13, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi ya Sahare katika Manispaa ya Tanga akitoa ushuhuda wake jinsi alivyoishi kwa kuvua samaki katika umri wake mdogo.
IMG_1357Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa chakula cha jioni cha kampeni za kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania kilichoandaliwa na International Rescue Committee kwenye Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.
IMG_1397Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi kampeni ya kadi nyekundu katika kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na International Rescue Committee katika Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.
PICHA NA JOHN  LUKUWI  

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!