Na Steven Augustino wa demasho.com, Tunduru
WATU
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia ofisi za wanunuzi wa madini ya vito ya RUBY and SAPPHIRE kutoka Srilanka, na kuwashambulia walinzi na wamiliki wa ofisi hizo kwa kutumia
silaha za jadi, na kufanikiwa kuiba kiasi cha Shilingi Milioni 10 na kisha kutoweka
kusikofahamika.
Taarifa
za tukio hilo zinaelezea kuwa sambamba na kiasi hicho cha pesa,
maharamia hao
walifanikiwa kuiba vifaa vya mawasiliano (IPAD) 3, zenye thamani ya Dola
za Kimarekani 240, sawa na Shilngi 384,000 za kitanzania.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Mihayok Msikhela, amesema kuwa katika
tukio hilo, majambazi hao waliwajeruhi watu watatu akiwemo mlinzi,
aliyefahamika kwa jina la
Rashid Ally (70) ambaye baadaye alifariki dunia wakati akipatiwa
matibabu katika
hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru.
Kamanda
Msikhela, aliwataja majeruhi ambao walipigwa na kuwakata na vitu
vianvyodhaniwa kuwa ni nondo na mapanga kuwa ni, wafanyabishara wa
kampuni hiyo ya ununuzi wa madini raia wa Srilanka, Bw. Mohammed Fathik
na Bw. Abudul Ifham, ambao baada ya
tukio hilo wameondoka kurejea nchini kwao kwa ajili ya matibabu.
Alisema
taarifa zinaeleza kuwa, mlinzi aliyekumbwa na mkasa huo marehemu Rashidi
Ali, alikuwa amemsaidia kazi hiyo ya kulinda mjomba wake, Bwana Musa
Adamu, ambaye alikuwa yupo katika
mapumziko ya siku mbli baada ya kuoa, katika ndoa iliyofanyika Agosti 31
mwaka huu.
Kamanda
Msikhela aliendelea kufafanua kuwa, kufuatia hali hiyo Polisi wilayani Tunduru
wanaendelea kukisaka kikundi cha maharamia hao, ili sheria iweze kufuata mkondo
wake.
Wakizungumzia
tukio hilo kaimu wa kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya serikali ya wilaya ya
Tunduru Dkt. Zabron Mmary na Muuguzi wa Zamu katika wodi namba moja, Bw. Koletah
Mnunduma Mtutura, walikiri kumpokea majeruhi huyo majira ya saa 10.30 za usiku
wa kuamkia September 2 mwaka huu na kwamba marehemu aliletwa Hospitalini hapo akiwa hajitambui, huku akiwa anatokwa na damu nyingi masikioni, puani na mdomoni.
Walisema
hata hivyo mzee huyo, alifariki dunia wakati juhudi za maafisa tabibu kuokoa
maisha yake zikiendelea.
Mganga
aliyeufamyia uchunguzi mwili wa marehemu Rashidi Ali, Dkt. Joseph Komba, alisema kuwa
chanzo cha kifo cha marehemu kimetokana na kutokwa na damu nyingi baada ya kupasuka
fuvu la kichwa, hali iliyosababisha damu kuchanganyika na ubongo.
CHANZO. DEMASHO BLOG
CHANZO. DEMASHO BLOG
No comments:
Post a Comment