Beyonce na Jay Z wapo njiani kununua na kuhamia kwenye nyumba ya kifahari yenye thamani ya dola milioni 85 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 141 huko Beverly Hills.
Nyumba hiyo ilijengwa na bilionea, Bruce Makowsky.
Nyumba hiyo ya kisasa yenye ukubwa futi za mraba 23,000 ina vyumba vinane, mabafu 15, bwawa la kuogelea, jumba la sinema lenye viti 24 na vingine. Kwa mujibu wa TMZ, Beyonce na Jay Z ambao walidaiwa kuwa na mgogoro wa ndoa yao, waliikagua nyumba hiyo walau mara mbili kabla ya kwenda kwenye ziara yao.
Tazama picha za nyumba hiyo.
CRD: BLOG YA WANANCHI.
No comments:
Post a Comment