Thursday 18 September 2014

ATHARI KATIKA MFUMO WA MKOJO:


Ni hali jnayojitokeza pindi mhusika anaposhindwa kupata haja ndogo kabisa au kupata kdgo lkn kwa maumivu makali.


Athari katika tezi ya prosteti hubana njia ya mkojo na kuifanya nyembamba zaidi.Ongezeko la mbinyo au ukinzani linafanya iwe vigumu zaidi kwa kibofu kutoa nje mkojo
ambapo kibofu kinajaribu kuishinda nguvu kinzani kwa kubana kwa nguvu kwa nguvu nyingi zaidi.Hili linasababisha kuongezeka kwa ukubwa wa tishu za kibofu.Kadri tezi ya protesti inavyoendelea kupanuka inaongeza ukinzani ktka njia ya mkojo,inasababisha ongezeko zaidi la nguvu za kukaza kibofu na hivyo kuongezeka zaidi kwa ukubwa wa kibofu.DALILI:-Mchirizi dhaifu wa mkojo-Kuziba mkojo ghafla-Kupata haja ndogo mara kwa mara-Kushindwa kuzuia hisia ya mkojo-Figo kushindwa kufanya kazi-Tumbo kuwaka moto chini ya kitovu/kinena-Maumivu makali ya mgongo,kiuno,nyonga inayopanda hadi begani..NB-Sababu kuu ya kupata mkojo mara kwa mara ni kibofu kushindwa kutoa mkojo wote na hivyo mkojo ulobaki unaachwa ndani ya kibofu na kuchukua mda mfupi kujaa hali inayosababisha hisia kali kutaka kukojoa.Kiujumla hali hii ya kuziba kwa mkojo huathiri utendaji wa kibofu na figo kwani shinikizo la ktka kibofu kilichotanuka linasababisha shinikizo kurudi nyuma mpaka kwenye mfumo wa juu wa mkojo'ureta na figo'hili linasababisha ureta kupanuka na figo kutanuka hatimaye figo inayochuja sumu kutoksa kwenye damu mwilini inaathirikã na kushindwa kufanya kazi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!