Saturday, 13 September 2014

ASILIMIA 52 YA WANAWAKE TANZANIA HUTUMIA VIPODOZI VYENYE SUMU


Zaidi ya asilimia 52 ya wanawake hutumia vipodozi vyenye sumu ambavyo huwasababishia matatizo mbalimbali ikiwamo kansa ya ngozi, figo pamoja na kuharibika kwa mimba kwa mama mjamzito. Aidha katika utafiti uliofanywa na Asasi isiyokuwa ya kiserikali Envirocare mwaka jana inaonyesha mikoa ambayo imeathirika zaidi na matumizi ya vipondozi hivyo ambayo ni Tanga, Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Kilimanjaro.





Meneja wa Mradi huo, Elfansia Shayo, alisema Envirocare imeandaa kampeni kwaajili ya kupinga matumizi ya vibodozi hivyo itakayofanyika leo jijini Dar es Salaam. “Envirocare kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imefanya utafiti ulionyesha zaidi ya asilimia 52 ya watumiaji wa vipodozi hivyo ni wanawake na baadhi yao wanajua madhara yake,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo, Loyce Lema, alisema kampeni hiyo inahusu kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi ya vipodozi hivyo na ambazo viambato hivi husababisha madhara kwa watumiaji na mazingira. Alisema pamoja na TFDA kuweka mfumo thabiti wa udhibiti wa vipodozi ambao unatumia njia mbalimbali ikiwamo usajili wa vipodozi, utoaji wa vibali vya biashara, na ukaguzi wa maduka bado mfumo huo unachangamoto kwani vipodozi vimekuwa vikiingizwa nchini kwa kutumia njia zisizo rasmi.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!