Waziri Mkuu wa Lesotho,Thomas Motsoahae Thabane, akihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa New York, Sept. 26, 2013.
Wanajeshi walishika doria kwenye mitaa ambayo ina majengo ya serikali na kuzingira makao rasmi ya Waziri Mkuu Thomas Thabane.
Waziri Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane amekimbilia Afrika Kusini kufuatia kile alichosema ni jaribio la kupindua serikali katika taifa hilo ndogo la kusini mwa Afrika. Mashahidi wanasema milio ya risasi ilisikika katika mji mkuu wa Maseru Jumamosi.
Wanasema wanajeshi walishika doria kwenye mitaa ambayo ina majengo ya serikali na kuzingira makao rasmi ya Waziri Mkuu Thomas Thabane. Bw. Thabane alisema hatua za jeshi ni sawa na mapinduzi ya serikali.
Alisema alikimbilia Afrika Kusini baada ya kupata habari za kijasusi kuwa analengwa kuuawa na majeshi. Katika mahojiano na Sauti ya Amerika, Waziri Mkuu huyo alisema tukio hilo lilitokana na ukosefu wa nidhamu katika jeshi.
Alisema ghasia hizo zinazongozwa na mwanajeshi wa zamani aliyekuwa katika cheo cha juu, ambaye aliondolewa kwenye wadhifa wake na serikali. Bw. Thabane amesema ataraejea nchini Lesotoho pale atakapokuwa na uhakika kwamba hatauawa. http://www.voaswahili.com
No comments:
Post a Comment