MKAMA SHAKENGWA NI KIONGOZI KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO WENYE ULEMAVU MBALIMBALI CHA BUHANGIJA WAKIWEMO ALBINO.
WATOTO wenye ulemavu wa ngozi katika kituo maalumu cha kulea watoto hao Buhangija manispaa ya Shinyanga ,wamezidi kuongezeka kituoni hapo kutokana na wimbi la mauaji y a albino kuibuka tena na kufikia watoto zaidi ya 100 kupelekwa hapo kutoka maeneo mbalimbali kwa hofu ya kuuwawa na kufanyiwa ukatili.
Pia watoto wengi wametoka kwenye mikoa ya Tabora,Simiyu na Mwanza ikiwa watoto wa kike 98 na wakiume 96 , baada ya mauaji hayo kuibuka tena tangu kwenye mwezi mei mwaka huu kwa kuuwawa mwanamke mmoja huko mkoani Simiyu na mkoani Tabora watu wawili kuuwawa kwa kipindi kifupi,ambapo kila siku watoto watatu mpaka wanne wanaletwa kituoni hapo.
Wakizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada iliyotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo, kupitia harambee iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali Easy flex la mjini Shinyanga kwa ajili ya kusaidia watoto hao huku mwalimu mkuu wa kituo hicho Peter Ajali akieleza changamoto za ukosefu wa sehemu ya malazi pia.
Baadhi ya watoto wa kituo hicho wanaosoma shule ya msingi Buhangija darasa la saba Rehema Masunga,Mkama Shakengwa na D walisema nchi ya Tanzania inasifika kwa kuwa na amani lakini sasa hali inaelekea kuwa mbaya kutokana na baadhi ya watu kuwa na roho za kikatili na kuuwa binadamu kama wanyama .
“Inasikitisha sana kuibuka tena mauaji ya albino tuliona kwenye vyombo vya habari watu wamekatwa mkono,naiomba jamii iwapuuze waganga wa kienyeji maana ndiyo wanachangia, tumuamini mungu atatuepusha na unyama huu wa kikatili”alisema Daniel Limbu.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye pia ni msimamizi wa kituo hicho Peter Ajali,alisema kufutia kutokea kwa matukio mawili ya albino kukatwa viungo vyao vya mwili mkoani Tabora na mmoja Bariadi kuuawa matukio hayo yamesababisha kuongezeka idadi ya watoto kituoni hapo hivyo kuwa na msongamano mkubwa.
AkizungumZa kwenye hafla hiyo meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamu Hafidhi aliitaka jamii kuwa na utamaduni wa kusaidia kituo hicho,badala ya kutegemea msaada kutoka kwa wafadhili huku akisisitiza mikoa yote iliyopeleka watoto kutoa michango itakayosaidia kukidhi mahitaji na kuwaomba kuielimisha jamii umuhimu wa kusaidia.
Awali mkurugenzi mtendaji wa Easy flex production Happness Kihama alisema changamoto kubwa iliyopo ni uelewa mdogo kwa jamii ,juu ya kusaidia vituo hivyo vyenye mahitaji maalumu wazee na walemavu kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali ,ikiwa ni pamoja na uchakavu wa majengo,chakula na malazi.

No comments:
Post a Comment