Tuesday, 26 August 2014

MIILI YA WATU 40 YAPATIKANA IKIELEA ZIWA RWERU

Miili yapatikana imeelea katika ziwa Rweru Burundi
Burundi imeanzisha uchunguzi baada ya miili ya watu kadhaa kupatikana ikielea katika ziwa la mpakani na nchi hiyo na Rwanda.
Miili hiyo iligunduliwa na wavuvi hivi majuzi.

Burundi imesema miili hiyo si ya raia wake ,Police wa Rwanda nao wametoa taarifa kukan kuwa miili hiyo ni ya wanyarwanda waliouawa nchini Rwanda na kutupwa ziwani humo.Haijajulikana watu hao waliuwa wapi na vipi .
Ripoti kuhusu miili hiyo ndio kwanza zaibuka lakini wenyeji waliokaribu na jiwa hilo la mpakani liitwalo Rweru wanasema walianza kuona miili hiyo tangu wiki kadhaa zilizopita.
Wameweka idadi ya miili hiyo kwa jumla ya 40 ikiwemo mitano iliyogunduliwa juzi na jana.
Afisa wa Burundi aliyekwenda kushuhudia anasema yeye binafsi ameiona baadhi ya miili hiyo iliyokuwa imefichwa kwenye mifuko miwili mikubwa.
Hata hivyo Afisa huyo , Jean Berchmans Mpabansi, amesema maiti hizo si za raia wa Burundi kwani ilifika eneo hilo ikielea kutoka mto Akagera unaotiririka kutoka Rwanda.
Waakilishi wa polisi wa Rwanda nao walikwenda eneo hilo pamoja na maafisa wa Burundi lakini nao wakasema hamna ripoti za watu kupotea nchini Rwanda.

Miili hiyo imepatikana ikiwa katika hali mbaya ya kuoza hivyo kuzua tatizo la kiafya kwani wakaazi hutumia maji ya mto huo kwa matumizi yao ya kila siku kwani sehemu hiyo ya mkoa wa Muyinga hukabiliwa na ukame wa mara kwa mara.
Nchi hizo mbili zimekubali kufanya uchunguzi kubaini ukweli wa tukio hilo.
BBC.

1 comment:

Anonymous said...



aziz bilal02:35


1
Reply

genocide nyingine yaja nchini Burundi,vipi tena muzee Nkurusinza mambo hayaonekani vizuri nchini kwako.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!