Taarifa kutoka Liberia zinasema kuwa kituo kilichotengwa na kuwekewa karantini kwa sababu ya ebola, kimeshambuliwa na zana kuibiwa mjini Monrovia.
Baadhi ya ripoti zinasema wagonjwa kadha wameondoka kituoni.
Tukio hilo limejiri katika mtaa wa shughuli nyingi uitwao West Point.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.
No comments:
Post a Comment