Tuesday, 15 July 2014

VIGOGO BANDARI MBARONI

Vigogo Bandari kizimbani
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Ephraim Mgawe na naibu wake, Hamad Koshuma, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana, wakikabiliwa na shitaka la kutumia madaraka vibaya.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Isaya Arufani, Mwendesha Mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ben Lincoln, alidai Desemba 5, 2011, kwa nyadhifa zao, washitakiwa hao walitumia vibaya madaraka kwa kusaini mkataba wa kujenga gati namba 13 na 14 pasipo kutangaza tenda, ikiwa ni kinyume na sheria ya manunuzi.
Lincoln aliendelea kudai kuwa washitakiwa hao walisaini mkataba huo na Kampuni ya China Communication Construction Limited, kwa nia ya kujipatia fedha zaidi kutoka kampuni hiyo.
Washitakiwa hao walikana shitaka hilo na wako nje kwa dhamana hadi Agosti 13, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Agosti 2012, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aliwasimamisha kazi vigogo saba wa TPA, akiwamo Mgawe na Koshuma kwa tuhuma za uhujumu uchumi na kukaidi maagizo ya Ikulu.
Tuhuma nyingine alizozitaja Dk. Mwakyembe ni pamoja na wizi wa kontena za wateja unaofanywa katika Kitengo cha Kontena (Ticts), udokozi wa mizigo na vitu mbalimbali vikiwamo vifaa vya magari, rushwa ndogo na kubwa na wizi wa mafuta katika kitengo cha KOJ.
Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe, uamuzi wa kuwasimamisha kazi vigogo hao, aliufanya baada ya kikao na Bodi ya Wakurugenzi ya TPA na kubaini kuwapo kwa vitendo viovu vilivyochangia kuhujumu uchumi wa nchi.
Mbali ya Mgawe na Koshuma, pia panga la Mwakyembe liliwakuta Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ng’amilo, Meneja wa Kurasini Oil Jetty, Meneja wa Jetty na Terminal Oil Engineer

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!