![](http://www.ippmedia.com/media/picture/large/loga-feb20-2014(2).jpg)
Kocha Mcroatia wa Simba, Zdravko Logarusic amesema fainali zilizomalizika za Kombe la Dunia zilikuwa na vitu vingi vya kujifunza kwa wachezaji wa Tanzania, hasa suala ya kujituma na nidhamu ya mchezo.
Logarusic alisema fainali za Kombe la Dunia zinatakiwa kuwabadilisha wachezaji wengi wa Tanzania ili kuifanya Ligi Kuu Bara kuwa na ushindani mkubwa.
Logarusic alisema wachezaji wengi katika michuano hiyo walionyesha soka la kiwango cha juu huku timu ndogo zikionyesha maajabu.
“Kulikuwa na vitu vingi vya kujifunza katika fainali hizo, ambazo mwaka huu zilikuwa na msisimko mkubwa. Hivyo kama wachezaji wangu walikuwa wakifuatilia naamini watakuwa wamepata kitu kitakachowasaidia kwenye ligi.
“Kikubwa ni nidhamu ya mchezo. Unaona kabisa wachezaji wanataka ushindi, wanajitolea uwanjani wanafuata maelekezo ya makocha wao, jambo ambalo kwa wachezaji wengi hapa halipo. Muda mwingine wanacheza tu,” alisema Logarusic.
3 comments:
aziz bilal03:10
1
Reply
Actually mimi naona hakuna cha kujifunza kwani hapa hapa kwetu tunashindwa kujiendeleza kisoka,ninamaanisha huku kwetu east africa na central Africa tunashindwa kila siku itakuwa kuchuana au kushindana na waafrica magharibi ambao wamefanya fainali za kombe la dunia kama ni wao ndio wanapaswa kuliwakilisha bara la Africa.Nahii rushwa huku kwetu,sijui ka tutaweza fikia level hiyo.yangu ni macho na masikio tuu
aziz bilal03:02
1
Reply
kazi nyingi sana za wasanii wa bongo wanadhulumiwa,sio Wema pekee karibu wote wanaibiwa kila kukicha
Post a Comment