MALKIA wa mipasho nchini, Khadija Kopa, amesema katika kuchanganya ladha ya muziki kwa wapenzi wake, amepanga kufanya kolabo na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, wakiwemo Alikiba na Diamond Platinumz.
Mbali ya hao, Kopa alisema pia anakusudia kufanya kazi na wasanii wengine kama, Ommy Dimpoz, Chid Benz na Cassim Mganga ili kuendelea kuwashika mashabiki wa kazi zake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Kopa alisema anachosubiri ni kwisha kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kabla ya kugeukia kazi hizo ambazo tayari ameanza maandalizi yake.
Aidha Kopa alisema yupo katika hatua za mwisho za maandalizi ya albamu zake mbili ambazo pia atazisambaza baada ya kwisha kwa mwezi huu.
“Nipo katika michakato ya kutoa albamu zangu mbili; moja inajulikana kwa jina la ‘Lady with Confidence’ na ‘Kantangaze akutangaze nani wakati hata mtaa wa pili haujulikani,” alisema.
Msanii huyo nguli anawasihi wapenzi wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya kupokea kazi hizo ambazo anaamini zitafanya vizuri kutokana na maudhui yaliyomo na ujumbe wake.
No comments:
Post a Comment