WANAMUZIKI na wadau wa muziki watakutana Alhamisi hii saa 5 asubuhi kujadili namna ya kusaidia na kushiriki mazishi ya mwimbaji Amina Ngaluma(Japanese).
Hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Vijana Social Hall (jirani na Mango Garden), Kinondoni jijini Dar es ambapo itaangaliwa namna nzuri ya kushirikiana na familia ya marehemu kuanzia hatua ya kuupokea mwili hadi mazishi.
Mwili wa Amina Ngaluma aliyefariki nchini Thailand Alhamisi iliyopita, utawasili jijini Dar es Salaam Ijumaa hii saa 3.30 usiku kwa ndege ya KLM. Mazishi yatafanyika siku inayofuata (Jumamosi) mchana.
Mmoja wa waratibu wa kikao hicho cha Alhamisi kinachoshirikisha pia Shirikisho la Muziki Tanzania, Mwinjuma Muumin, amesema msiba huu umechukua muda mrefu, familia imeingia gharama kubwa katika kipindi chote hiki na hivyo ni wakati muafaka sasa kwa wanamuziki na wadau wa muziki kukutana na kuangalia namna ya kuipunguzia mzigo familia ya marehemu.
Muumin amesema kuna mambo mengi ya msingi ya kujadiliana katika kikao hicho na kwamba taarifa zote muhimu za mazishi ya Amina Ngaluma zitatolewa hapo.
Mwanamuziki Rashid Sumuni ambaye ni mume wa marehemu anatarajiwa kuhudhuria kikako hicho.
Naye Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo November amesema kikao hicho ni muhimu na kitafungua njia ya umoja na mshikamano miongoni mwa wasanii hususan wanamuziki wa dansi
No comments:
Post a Comment