Wednesday 28 May 2014

WALIOTEKA MABASI TABORA KUNYONGWA


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora, imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu wawili waliokamatwa wakimiliki silaha mbili za kivita na sare zinazotumiwa na jeshi la nchi jirani ya Burundi bada ya kutiwa hatiani kwa kosa la mauaji.
Waliohukumiwa ni Charles Ngwandu (Mpikachai) na Shaban Mabala (Mwanamswaya).


Akitoa hukumu hiyo, Jaji Amir Mruma, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.
Awali, upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili Edward Mokiwa na Juma Masanja, ulidai Oktoba 27, mwaka 2008, saa 2 asubuhi, eneo la Isenefu wilaya ya Uyui mkoani hapa, washitakiwa waliteka mabasi mawili yaliyokuwa na abiria T 273 AMT mali ya kampuni ya Suden Classic na T 153 AQC mali ya kampuni ya Comb Truck.
Walidai katika tukio hilo walifyatua risasi tano na kumuua papo hapo abiria mmoja Athumani Mohamed, na mwingine Shaban Masoud alifia hospitali ya Mkoa Kitete. Pia Hawa Said ambaye alikuwa ni miongoni mwa abiria alifariki kwa mshutuko baada ya kusikia milio ya risasi.
Akitoa utetezi wake kabla ya kutolewa kwa huduma huyo, Mpikachai alidai ni mwathirika wa Ukimwi huku mwenzake akidai anasumbuliwa na ugonjwa wa Pumu.
chanzo; Tanzania Daima

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!