Wednesday, 7 May 2014

MPANGO WA KUTOA HUDUMA PAMOJA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZWA WAJA

2Na  Magreth Kinabo- Maelezo
Serikali inaandaa mpango wa kutoa huduma za magonjwa yasiyopewa kipaumbele(NTD,s) kwa pamoja ili kuweza kufikia watu wengi kwa kupunguza gharama.

Hayo yamasemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma  za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila wakati akifungua mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa  kipaumbele leo unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
“ Tumekutana na wadau mbalimbali katika mkutano huu lengo ni  tunataka kuandaa mpango wa  kutoa huduma na dawa kwa magonjwa yasiyopewa kiupaumbele kwa pamoja badala ya ugonjwa mmoja pekee.Tunaweza kupata matokeo zaidi na kusaidia  kuwafikia  watu wengi  kwa kuwa utarahisisha utendaji kazi, utoaji elimu na dawa,” alisema Dk. Neema.
Dk. Neema aliyataja magonjwa hayo kuwa ni Usubi, Trakoma, Kichocho, Minyoo, Mabusha na Matende.
Aliongeza kuwa  hivi sasa huduma hiyo imeweza kufikia  wilaya 108  kati ya 160.Hivyo  changamoto iliyopo ni kufikia mikoa saba.
Alisema mpango huo ulianza mwaka 2012 na unaendelea hadi mwaka 2017, ambapo mafanikio yameonekana mfano katika kupambana na ugonjwa wa usubi utafiti ulifanyika umeonesha kuwa kati ya wilaya tisa ni wilaya mbili ndizo zitaendelea kupatiwa dawa.  
Naye Meneja Mpango  wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele(NTD,s),Dk, Upendo Mwingira alisema changamoto nyingine iliyopo katika kubabiliana na magonjwa hayo ni baadhi ya jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya magonjwa hayo ambayo dalili zake si rahisi kuonekana kwa macho  kwani huonekana baada ya muda mrefu mfano Matende na Mabusha.
Alisema  baadhi ya jamii   huwa mwitiko mdogo  wakati wa utoaji wa huduma, hivyo Dk. Upendo aliitaka jamii kujitokeza kwa wingi wakati wa utoaji wa huduma hizo.
 Alizitaja  baadhi ya athari ya magonjwa hayo kuwa ni ulemavu wa kudumu na miongoni mwa sababu zinazochangia kuwepo kwa matataizo hayo ni umasikini.
 Dk. Upendo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!