Wednesday 28 May 2014

DHAHABU YA SAMUNGE NI "ALLUVIUM"


‘Dhahabu ya Samunge ni Alluvium’
KAMISHNA wa  Kanda ya Kaskazini, Alex Mayagane, amethibitisha kuwa madini yanayochimbwa kwenye Kijiji cha Mgongo, wilayani Ngorongoro ni dhahabu aina ya ‘alluvium’ .


Alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa taarifa ya awali ya timu ya wataalamu wake waliokwenda kufanya utafiti kwenye eneo hilo maarufu kama Kwa Babu wa Loliondo baada ya kuzagaa kwa taarifa kuwa linapatikana dhahabu hivyo kuvuta watu kutoka maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa wataalamu hao wanatarajiwa kurudi kijijini Mgongo mapema wiki hii kwenye eneo linalochimbwa dhahabu ili watafiti miamba kwa lengo la kubainisha dhahabu imeenea kiasi gani.
Mayagane alisema kuwa matokeo yatakayopatikana watawasiliana na Wizara ya Nishati na Madini kwa lengo la kupendekeza maeneo hayo yatengwe kwa uchimbaji mdogo mdogo kwani tayari kuna viwanja 16 vilivyokwisha pimwa na wachimbaji wadogo wanaendelea kufanya kazi kwa ushirika.
Alisema watawasiliana na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro yalipobainika madini hayo kuona namna gani wanaweza kupata ushuru kwa kuwa madini ni mali ya serikali.
Mkuu wa wilaya hiyo, Elias Wawa Lali, mwishoni mwa wiki aliwaeleza waandishi wa habari kuwa anasubiri matokeo ya utafiti huu ili kuiwezesha serikali kutoa muongozo juu ya namna ya kuyachimba ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza endapo watu wataachwa kuchimba holela kama ilivyo sasa.
Alisema kuwa serikali imeimarisha ulinzi kwenye eneo hilo kwa kuongeza mgambo wa kutosha na polisi, sanjari na kuboresha mazingira ya eneo husika kuhakikisha huduma muhimu za vyoo zinapatikana ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kama wakati wa kupata ‘kikombe cha babu’

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!