Tuesday 1 April 2014

ZAIDI YA WAWEKEZAJI 65 WANATARAJIWA KUWEKEZA NCHINI

ZAIDI ya wawekezaji 65 wanatarajiwa kuja nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo viwanda na utalii.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alibainisha hayo jijini Dar es Salaam juzi alipokuwa  akielezea ziara iliyofanywa na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dk. Frank Walter na baadhi ya wawekezaji hao.

Alisema ujio huo umekuwa na manufaa kwani wameahidi kukarabati Reli ya Kati pamoja na kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea Mkoa Mtwara, ili kuwasaidia wakazi wa mkoa huo kupata mbolea kwa urahisi.
“Wawekezaji hawa watawekeza katika sehemu mbalimbali ila watajikita zaidi katika Mkoa wa Mtwara na kujenga kiwanda hicho kikubwa kuliko vyote katika ukanda wa Afrika Mashariki, hiyo ni kutokana kwa kugundulika kwa gesi ambayo itawasaidia katika kukuza uchumi wa nchi,” alisema.
Kwa upande wake, Dk. Walter alisema kutokana na mahusiano mazuri baina ya nchi hizo ambao umedumu takriban miaka 50 ni ishara tosha ya kuleta maendeleo na wataendelea kuisaidia kwa kuleta wawekezaji wengi zaidi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!