Tuesday 1 April 2014

UTURUKI KUSHIRIKI MIRADI YA UJENZI NCHINI

Orhan Babaoglu na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli
KAMPUNI tatu kutoka Uturuki zimeingia nchini kwa lengo la kushiriki katika ujenzi kwenye miradi tofauti katika maeneo mbalimbali.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA ya Uturuki, Orhan Babaoglu, alisema kukua kwa sekta ya ujenzi nchini ndicho kigezo kilichowafanya wafungue ofisi zao.

Akizungumza kwa niaba ya Kampuni ya Bosandra Professional Co. Ltd , Babaoglu alimpongeza Waziri wa Ujenzi, John Magufuli kwa kusimamia sekta hiyo hadi kampuni kutoka Uturuki kufungua ofisi zao nchini.
“Tumekuwa tukifuatilia uendeshwaji na ukuaji wa sekta ya ujenzi katika mataifa mbalimbali barani Afrika na tumejiridhisha kuwa Tanzania  ni nchi inayofanya vizuri katika upande huo,” alisema Babaoglu.
Mwakilishi  mwingine wa Kampuni ya CEYTUN, Kursat Durak, alisema utendaji wa kampuni kutoka Uturuki unafahamika duniani  kote, hivyo ujio wao una lengo la kuamsha ushindani wa ubora lakini pia kuona gharama za utekelezaji wa miradi hiyo zinadhibitiwa kwa kuwa na washindani kutoka maeneo tofauti.
Waziri Magufuli alisema hivi sasa kuna miradi mbalimbali inayokusudiwa kuendeshwa kwa kushirikiana na sekta binafsi, hivyo ni fursa kwao pia kuangalia maeneo yatakayowavutia.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!