Wednesday, 2 April 2014

TYLER PERRY KUSAKA VIPAJI VYA WASANII WA FILAM TANZANIA

Tyler-PerryMsanii maarufu na mcheza sinema wa Marekani Tyler Perry ametangaza kwenda nchini Tanzania hivi karibuni mahsusi kwa ajili ya kutafuta vipaji vya wasanii wa Tanzania kwa upande wa filamu.
Safari hii ilitangazwa kwenye jarida moja la huko Atlanta Georgia yaliko makao makuu ya studio maarufu na za aina yake za Tyler Perry.


KILICHOMVUTIA
Tyler Perry amenukuliwa kuvutiwa na usanii wa waafrika halisi ambao anataka sana kufanya nao kazi katika filam zake ili aweke kupata vionjo vya kiafrika katika filam zake. Kwa upande wa Bongo Moies Wasanii aliovutiwa nao alisema ni pamoja na Rich Mavoko, Jacob Steven (Jb), Aunt Ezekiel na Shilole.
Katika kampeni yake hiyo hiyo Tyler Perry atashirikiana na kampuni ya kutafuta vipaji(scouting) yenye makao yake Atlanta Classie Entertainment Agency yenye sifa kubwa ya kuibua vipaji vya pekee hapa Marekani.

CRD: SUNDAY SHOMARI BLOG

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!