Wednesday, 2 April 2014

SHEIKH ABOUBAKAR MAKABURI AUAWA

DN+COAST+MAKABURI+2703D.JPGHali inaelekea kuwa ni ya wasi wasi huko Mombasa baada ya kifo cha shekhe Abubakar Makaburi ambaye alikuwa amewekewa vikwazo na Marekani na umoja wa mataifa kwa msimamo wake wa kuunga mkono kundi la alShabab.

Mauaji hayo yaliofanywa na watu wasiojulikana wenye silaha yametokea baada ya serikali ya Kenya kutangaza imeanza operesheni ya kuzuia wimbi la mashumbilizi nchini humo wakati maafisa wamekamata zaidi ya watu 650 huko Nairobi kufuatia shambuliz la bomu jumatatu.
Wakili Mbugua Muriethi amesema shekhe Abubakari Sharrif “Makabur” aliuwawa pamoja na mtu mwingine asiyejulikana karibu na jele ya shimo la Tewa katika mji wa Mombasa.Mauaji hayo yanatishia kuleta ghasia za kulipiza kisasi.
Shekhe Ahmed wakati wote alikuwa akisema yuko hatarini kuuwawa na askari wa usalama Muriethi aliongeza.Amesema Ahmed alianza kutoa madai hayo mara baada ya yeye na Mohamed karibu wakamatwe nje ya mahakama moja huko Nairobi Julai 2012.
Mureithi anasema mahojiano yake ya mwisho na TV nchini humo ambapo alionekana kuunga mkono mauaji ya raia katika mall ya Nairobi yanaweza kuwa yamechangia kifo chake.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!