Wakazi wa kata ya Msinjahili wilayani Lindi wametakiwa kutoogopa kuvuta umeme majumbani mwao kwa kuhofu kuwa wakifanya hivyo wataonekana ni matajiri kwani matumizi ya umeme ni ya gharama naafuu ukilinganisha na mafuta ya taa.
Mwito huo umetolea jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) wilaya ya Lindi mjini wakati akiongea kwa nyakati tofauti na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho katika matawi ya Muungano, Jitegemee, Sinde na Mnali yaliyopo katika kata ya Msinjahili wilaya ya Lindi mjini.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema ili kuboresha maisha ya wananchi Serikali imejitahidi kupitisha umeme wa gesi katika vijiji vilivyopo katika kata hiyo na kupunguza gharama ya uvutaji ambazo ni nafuu jambo la muhimu ni kwa wananchi kuutumia.
“Kuwa na umeme nyumbani kwako na kuutumia ni mwanzo wa maendeleo, hata watoto wako wataweza kuutumia mwanga huo kwa kujisomea hasa nyakati za usiku na hivyo kufanya vizuri katika mitihani yao”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mjumbe huyo wa NEC pia aliwataka viongozi hao wa Halmashauri kuu ya tawi kuwahimiza watu wanaowaongoza katika maeneo yao kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kulima chakula cha kutosha jambo ambalo litawafanya kuwa na chakula cha ziada na hivyo kuepukana na kitendo cha kuomba chakula kwa majirani.
Akizungumzia kuhusu suala la uongozi Mama Kikwete aliwahimiza wanawake kutoogopa kuomba na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo ili waweze kupata nafasi ya kuongoza na hivyo kufika katika ngazi ya maamuzi.
Mama Kikwete alisisitiza , “Sisi wanawake tunakabiliwa na changamoto nyingi na mtu pekee anayeweza kuziongelea changamoto zetu kiusahihi ni mwanamke mwenyewe hivyo basi msiogope kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati wa uchaguzi ukifika mkifanya hivyo kutakuwa na viongozi wengi wanawake ambao wataweza kuwakilisha matatizo na mawazo yetu katika ngazi za juu za uongozi wa chama na Serikali”.
MNEC huyo alimalizia kwa kuwahimiza viongozi hao wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM kuishi maisha ya upendo, mshikamano na amani kwani jamii ikiishi maisha hayo itaweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana.
MNEC huyo alimalizia kwa kuwahimiza viongozi hao wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM kuishi maisha ya upendo, mshikamano na amani kwani jamii ikiishi maisha hayo itaweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana.
Kwa upande wake katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Lindi Haji Tajiri aliwataka viongozi hao kuwa waaminifu katika ndoa zao na kuepuka tabia ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja (michepuko) kwa kufanya hivyo wataepukana na ugonjwa wa Ukimwi.
“Chama Cha Mapinduzi kinahitaji kuwa na watu wenye afya njema ili waweze kufanya vizuri kazi za chama nawaomba muwe waaminifu kwa wapenzi wenu mkifanya hivyo mtaepekana na Ugonjwa wa Ukimwi”, alisema Tajiri.
Katibu huyo wa Jumuia ya Wazazi mkoa pia aliwaomba kinamama kuiga mfano wa Mama Salma Kikwete ambaye anafanya kazi kubwa ya kujitoa katika shughuli mbalimbali za kijamii na kutetea haki zao, wasichana na watoto na kuongeza kwamba anastahili pongezi kwani yeye ni mama na mlezi wa taifa.
Mjumbe huyo wa NEC taifa akiwa katika kata ya Msinjahili alifungua mashina ya wakereketwa wa CCM Jumuia ya wazazi katika tawi namba tatu la Sinde na namba mbili la Mnali.
Mjumbe huyo wa NEC taifa akiwa katika kata ya Msinjahili alifungua mashina ya wakereketwa wa CCM Jumuia ya wazazi katika tawi namba tatu la Sinde na namba mbili la Mnali.
Mama Kikwete ambaye ni mjumbe wa NEC Taifa kupitia wilaya ya Lindi mjini alikutana na viongozi hao wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM kwa ajili ya kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na viongozi
No comments:
Post a Comment