Tuesday 22 April 2014

MAJAMBAZI YAKIWA NA BUNDUKI, MAPANGA (SMG ) YANASWA!


Majamabazi walionaswa wakiwa na bunduki aina ya SMG  haipo pichani
wakishushwa kutoka katika gali chini ya ulinzi wa askali kanzu waliopo
pembeni mwao.

-----------------------
Na Steven Augustino wa demashonews, Tunduru
Mkuu wa Kituo kidogo cha Matemanga F 1678 Cpl. Gwalugano kwa
kushirikioana na asikali polisi wenzake watano wamewakata Majambazi
wawili wakiwa na Bunduki aina ya SMG ambayo hadi sasa namba zake bado
hazijafahamika.





Aidha katika tukio hilo pia watuhumiwa hao walinaswa wakiwa na Risasi
19 magazini  ndani ya, Vifaa viwili vya kuficha sura (Maski) pamoja na
Vifaa mbalimbali na silaha za kijadi vilivyo ashilia kuwa maharamia
hao walijiandaa kwenda kufanya tukio la kinyama.


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamukia April 11, 2014 katika Kijiji
cha Kiuma nje kidogo ya Kituo hicho kilichopo katika Tarafa ya
Matemanga Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma ambapo pamoja na kukutwa na
vifaa hivyo majambazi hao pia walikutwa waikiwa na Mapanga
mawili,makoti mazito mawili na Tochi moja ya kujifunga kichwani.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Bw. Akili Mpwapwa amewataja
majambazi hao kuwa ni  Rashid Anafi (34) na Akimu Jafari (32) Wayao
wakazi wa Mtaa wa Ruvuma Mjini Songea.


Kamanda Mpwapwa aliendelea kufafanua kuwa Majambazi hao walinaswa
kufutia taarifa zilizotolewa na wasamalia wema na kwamba katika tukio
hilo watuhumiwa hao walinaswa wakiwa wanasafiri kutoka Mjini Songea
kuelekea mjini Tunduru kwa kutumia pikipiki aina ya Snlg yenye namba
za usajiri T 725 Cpu.


Alisema kufuatia hali hiyo watuhumiwa hao watahamishwa katika kituo
kikubwa cha Polisi cha Wilaya yaTunduru kwa ajili ya mahojiano zaidi
na baadae kufikishwa Mahakamani ili sheria iweze kufuata mkondo wake
kuanzia wiki ijayo.


Pamoja na kuwapongeza wananchi waliofanikisha kukamatwa kwa maharamia
hao pia ametoa wito kwa wananchi kuendele kutoa ushirikianao kwa jeshi
la polisi ili kudhibiti matukio ya uhalifu ambayo yanaweza kusababisha
madhara miongoni mwao.


KWA HISANI YA DEMASHO BLOG..

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!