Friday, 18 April 2014

Kumtukana Hayati Nyerere,Rais Kikwete anasema: "Ni kukosa adabu, Tuwaache walivyo, Dunia itawafundisha"


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ni ukosefu wa adabu kuwatukana waasisi wa Tanzania - JK

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
 Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni utovu wa nidhamu
 na ukosefu wa adabu kuwa baadhi ya Watanzania kuwatukana,
 kuwadhihaki na kuwakejeli Waanzilishi ma Taifa la Tanzania,
 Hayati Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume. 

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa viongozi hao wawili
 wameifanyia Tanzania mambo mengi, mambo makubwa
 na mambo ya kihistoria kiasi cha kwamba Watanzania
 wanao wajibu wa kudumisha na
kuenzi heshima yao kwa namna ya kudumu. 

Akizungumza na Wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari usiku 
wa jana, Jumatano, Aprili 16 katika mahojiano maalum ya kuadhimisha
 Miaka 50 ya Muungano, Rais Kikwete amesema: "Ni kukosa
 adabu na ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Mtanzania 
yoyote kuwatukana, kuwadhihaki ama kuwakejeli waasisi 
wa Tata letu. Hawa ni watu ambao waliifanyia nchi yetu
 mambo makubwa," amesema Rais Kikwete na kuongeza: 

"Mzee Karume yule aliongoza Mapinduzi yaliyoondoa
 dhuluma na uonevu pale Visiwani. Waafrika walio wengi
 walikuwa wanaonewa sana pale Tanzania Visiwani, pengine
 watu wamesahau, lakini hata pale walipokuwa wanashinda
 uchaguzi bado walikuwa hawapewi nafasi ya kuongoza 

maisha yao wenyewe." 

Amesisitiza Rais Kikwete: "Ni ukosefu wa adabu kwa yoyote
 kumshutumu mtu aliyejitolea kiasi hicho ili kubadilisha
 mfumo dhalimu na kujenga maisha na mazingira ya maisha

 bora kwa wengi." 

"Mzee Nyerere yule ametuachia Taifa moja, lililoungana, lenye
 umoja, lenye amani na mshikamano. Misingi ambayo aliijenga 
yeye ndiyo imeendelea kuongoza Taifa letu kwa miaka pate

 hii. Viongozi wengine wale ambao wamemfuata yeye —
 Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na sasa mimi mwenyewe,
 tumefuata na kuongozwa na misingi hii. Na siku
 nchi yet inaamua kuipuuza misingi hiyo, tutaingia
 katika matatizo makubwa." 

Rais Kikwete ametoa msimamo boo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu 
matusi, kejeli, dhihaki ambazo zimekuwa zinaonyeshwa na wajumbe
 wachache ma Bunge Maalum la Katiba juu ya waasisi hao ma
 Tanzania na Wabunifu Wakuu wa Muungano wa Tanzania. 

Imetolewa na: 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM, 
17 Aprili, 2014

CRD. MWIGULU NCHEMBA BLOG

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!