Taarifa bado zinazidi kutoka juu ya kile kivuko ambacho kilizama kikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi,taarifa zilizopo ni kwamba msaidizi wa tatu wa nahodha wa kivuko kilichozama anayeitwa Sewol ndiye aliyekuwa akiendesha kivuko hiko wakati kikizama.
Uchunguzi wa kina umebaini kuwa Nahodha mkuu haijabainika alikuwa wapi wakati wa tukio hilo ingawa inadhaniwa kivuko hiko kiligonga mwamba na kupinduka kwa haraka baada ya shehena yake kuegemea upande mmoja.
Wachunguzi sasa wanaelekeza juhudi zao kubaini kwanini Nahodha wa Sewol hakuwa kwenye usukani na pia kwanini baada ya tukio la kwanza abiria walikatazwa wasiruke baharini ili kuokoa nafsi zao kama ilivyo kawaida ya chombo kikipatwa na hali hiyo.
Leo asubuhi Waokoaji wamefanikiwa kuingia ndani ya kivuko hicho kilichozama baada ya kutoboa shimo upande wa juu wa kivuko hiko,kiongozi wa Mashtaka ya umma nchini Korea bwana Park Jae-Eok amesema kuwa nahodha mkuu Lee Joon-seok atakuwa na swali la kujibu.
Mpaka sasa abiria 270 waliokuwa ndani ya feri hiyo hawajulikani walipo asilimia kubwa kati yao wakiwa ni wanafunzi waliokuwa wakieleka katika kisiwa cha Jeju kwa safari ya masomo,watu 26 pekee ndio wamethibitishwa kufariki huku 179 wakitangazwa kuokolewa.
Imeandikwa na Bbc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment