Wednesday 16 April 2014

IDADI YA WALIOFARIKI KWA MAFURIKO ZAFIKIA 25, MAITI NYINGINE ZA WATU WANNE ZAPATIKANA



MAITI za watu wanne waliofariki dunia kutokana na mafuriko yaliyokumba maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam zimepatikana.
Maiti hizo zinafanya jumla ya watu walioripotiwa kufariki dunia kutokana na mafuriko hayo hadi sasa kufikia 18.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi, alisema jana kuwa juzi, maeneo ya Kivule daraja la Mto Mzinga na Kariakoo-Jangwani, ilipatikana miili ya watu wawili.
Alisema watu hao wametambuliwa kuwa ni Dunia Matandi (23), kondakta wa daladala maeneo ya Kivule na Frank Bwashehe, mkazi wa Jangwani.
Alisema kwa mujibu wa mashuhuda, Aprili 13, Matandi wakati akijaribu kuvuka daraja la mto huo aliteleza na kusombwa na maji ya mvua na hakuonekana hadi mwili wake ulipoonekana juzi. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika tukio jingine, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura, alisema mwili wa Elifaza Zakayo (65) mkazi wa Ubungo, juzi ulikutwa maeneo ya Mabibo External, Bonde la Mchicha.
Alisema kwa mujibu wa mashuhuda, wakati mvua inanyesha Zakayo alikuwa akijaribu kuokoa mali zake, lakini kwa bahati mbaya aliteleza na kuanguka na kusombwa na maji na hakuonekana hadi ulipokutwa mwili wake. Maiti  imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.
Mwili wa Juma Hassani (43), umeonekana ukiwa umeharikika maeneo ya Mto Mzinga-Mbagala.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema maiti hiyo ilikutwa juzi.
Kwamba Hassan alikutwa na umauti wakati akijaribu kuokoa mali zake wakati mvua ikinyesha. Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Temeke.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!