Tuesday 1 April 2014

AJALI RUFIJI TENA! WAKULIMA 7 WAHOFIWA KUFA MAJI

WAKULIMA saba wanahofiwa kufa maji baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kutoka Utete kuelekea Mkongo kupigwa wimbi na kugonga boti kisha kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea juzi saa 11 jioni katika Kivuko cha Utete wilayani Rufiji, mkoani Pwani ambapo mtumbwi huo uliokuwa na abiria 16.

Picha hii haihusiani na habari husika.

Akizungumza na Tanzania Daima,  Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurudin Babu, alikiri kutokea kwa ajali hiyo na kusema wakulima hao walikuwa wakitoka shambani katika Kata ya Utete.
Babu aliwataja waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Prisca Kulwa (20),  Diana Kulwa (14) Husina Mussa (13), Zambina  Mussa (8) Uwezo Mbonde (7) Zaria Mbonde (14) na Latifa Kibega (16).

Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni naodha wa mtumbwi huo, Abdallah Yusuph (22), Ramadhani Mkono (22), Nasira Magimba, Pili Hungwa, Shabani Mbonde, Ramadhani Gido, Khareem Salemu na Halid Mbonde.
Babu alisema majeruhi hao baada ya kuokolewa walipelekwa katika Hospitali ya Utete kwa matibabu zaidi na kuongeza kuwa hivi sasa majeruhi hao wameruhusiwa kutoka.
Alisema nahodha wa mtumbwi huo anashiliwa katika Kituo cha Polisi Utete kwa mahojiano zaidi huku akisisitiza kwamba tayari maiti ya mkulima mmoja imepatikana na juhudi za kutafuta maiti nyingine zinaendelea.
Alisema anawaomba wakulima wanaoenda kulima katika Mto Rufiji kipindi hiki cha mvua wawe makini kwa kuwa hali ya hewa ni mbaya.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba jeshi lake linamshikilia nahodha wa mtumbwi huo.
Kamanda Matei alisema ajali hiyo ilitokea siku moja baada ya ajali ile iliyosababisha vifo vya watu 21 huku wengine tisa wakiendelea na matibabu kwenye Zahanati ya Mchukwi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!