Wednesday 2 April 2014

627 WAKAMATWA BAADA YA SHAMBULIZI KENYA

Polisi nchini kenya wanasema kuwa wamewakamata zaidi ya watu 627 kufuatia mashambulizi ya hapo jana Jijini Nairobi ambapo takriban watu sita waliuawa.

Mkuu wa polisi David Kimaiyo alisema kuwa 200 kati ya watu hao ni watu wanaounga mkono kundi la Al Shabaab
Watu hao wote walikamatwa katika mtaa wa Easleigh na viunga vyake.
Watu 25 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo matatu yaliyotokea kwa wakati mmoja katika mtaa wa Eastleigh ambapo raia wengi wa kisomali wanaishi na kufanya kazi.
Polisi wanasema kuwa milipuko hiyo iliyotokea katika mikahawa miwili midogo huenda ilisababishwa na magurunedi pamoja na mabomu la kujitengezea.
Kumekuwa na mashambulizi kadhaa mjini Nairobi pamoja na mjini Mombasa katika miezi ya hivi karibuni ,ambapo polisi wanawalaumu waislamu wenye itikadi kali.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!