Afisa uhamiaji wa nchi ya Zanzibar amewataka watanganyika wanaokaa katika nchi hiyo wachukue vitambulisho vya muda vya ukazi, vinginevyo watahesabika kama ni wahamiaji haramu na wanaweza wakafurushwa kurudishwa nchini mwao Tanganyika wakati wowote.

Amesisitiza kwamba katiba ya Zanzibar inatamka wazi kwamba watanganyika wanaoishi Zanzibar sharti wawe na vitambulisho vya ukazi vya muda.

Amewataka watanganyika wasiokuwa na vibali hivyo, waende ofisi za uhamiaji zilizo karibu na mahali wanapoishi wakaombe vibali hivyo.

Source: Radio One News Bulletin—20th March, 2014.