Wednesday, 26 March 2014

TEKNOLOJIA ZA KISASA ITAONDOA CHANGAMOTO YA SEKTA YA UJENZI NCHINI

 
Bodi ya Usajili ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Ujenzi (AQSRB) imesema , utumiaji wa teknolojia ya kisasa katika sekta ya ujenzi ni jibu la uhakika la changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya maendeleo ya miundombinu Tanzania.
Bodi hiyo sasa imejikita katika mkakati madhubuti wa kuwashawishi wasanifu majengo, wakandarasi, wakadiriaji ujenzi na wadau wengine katika sekta ya ujenzi kuhakikisha inatumia teknolojia ya kisasa katika kazi zao ili kuboresha maendeleo ya miundombinu nchini.
 Akizungumza wakati wa warsha ya 21 ijulikanayo kama Continuing Professional Development (CPD), iliyodhaminiwa na Benki ya Exim Tanzania kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benjamin Mkapa mkoani hapa, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dk. Arch Ambwene Mwakyusa alisema, bodi kwa kutambua changamoto zinazoikabili Sekta ya Ujenzi Tanzania  ambazo ni pamoja na kuporomoka kwa majengo yanayojengwa na yaliyomalizika, inafikiri utumiaji wa teknolojia za kisasa zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ubora katika kazi zinazofanyika.
Dk. Mwakyusa alisema sasa msisitizo umewekwa kwenye matumizi ya teknolojia za kisasa  hususan kwa wasanifu majengo na wakadiriaji ujenzi kwa lengo la kuboresha ubora wa majengo nchini. “Tumesisitiza vya kutosha umuhimu wa kutumia teknolojia hizi mbili kwa wasanifu majengo na wakadiriaji ujenzi kwa sababu tunaamini kwa kupitia teknolojia hizi, tutaweza kuboresha majengo 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!