JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 022-2110146/2110150/2211679, Faksi: 022-2113271 Tovuti: www.moe.go.tz
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’ NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anatangaza nafasi za Mafunzo ya Ualimu ngazi yaCheti na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2013/2014 kama ifuatavyo:
A: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’: MUDA MIAKA 2
UALIMU: KAWAIDA
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2008 na 2012 na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua daraja la IV alama 27 katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja Au
-Awe na ufaulu kwa kiwango cha alama C katika masomo manne tofauti katika Mtihani wa Kidato cha
IV ulioyofanyika katika vikao zaidi ya kimoja.
-Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya ‘Mathematics’, ‘Biology’, ‘Physics’, ‘Chemistry’,
‘English’ na Kiswahili;
-Mwombaji aliyehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2012 hiyo ni sifa ya nyongeza.
UALIMU: MICHEZO
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2008 na 2012 na kufaulu Kidato cha IV kwa
kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.

-Mwombaji aliyehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2012 na mwenye uzoefu katika kufundisha
michezo (uthibitisho uambatishwe) ni sifa ya nyongeza.
UALIMU: ELIMU YA AWALI
-Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2008 na 2012 na kufaulu Kidato cha IV kwa
kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27 kwa Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja; na
-Mwombaji aliyehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2012 ni sifa ya nyongeza.
B: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA:- MUDA MIAKA 2
UALIMU:- MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII, BIASHARA NA LUGHA.
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2013 na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja.
- Awe mhitimu wa mafunzo mbalimbali katika ngazi ya NTA level 5 kutoka katika chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
1.
Tanbihi: Masomo ya ‘Economics’, ‘Basic Applied Mathematics’, ‘General Studies’, ‘Islamic
Knowledge’ na ‘Divinity’ hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji.
2
UALIMU: MICHEZO, MUZIKI, SANAA ZA UFUNDI NA SANAA ZA MAONESHO.
- Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2008 na 2013 kwa kiwango kisichopungua
‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja kwa kuzingatia masomo yafuatayo kwa kila kozi:-
Sanaa za Ufundi: masomo ya ‘Fine Art’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha IV masomo ya ‘Biology,
History, Physics, English, na Civil Engineering’
Sanaa za Maonesho: masomo ya ‘Thearte Arts’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha IV masomo ya
‘Literature in English, Kiswahili, Geography na History;
Muziki: masomo ya ‘Music’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha IV masomo ya ‘English, Kiswahili,
Music, Physics, Geography na History’; na
Elimu kwa Michezo: masomo ya ‘Physical Education’ pamoja na ufaulu wa Kidato cha IV masomo
ya Biology, Chemistry, Physics, English’ na Kiswahili.
UALIMU: UFUNDI
- Mwombaji awe amehitimu mafunzo ya FTC kati ya mwaka 2008 na 2013 kutoka vyuo vya Ufundi
Au awe amehitimu mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA level 6 kutoka chuo chochote cha Ufundi
kinachotambulika na Serikali.
UALIMU: KILIMO

“Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja katika somo la ‘Agricultural Science’ na ‘Biology’
Au ‘Chemistry’.
UALIMU: SAYANSI KIMU

kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika masomo ya ‘Biology’,
‘Chemistry’ na ‘Nutrition’.
C: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI NGAZI YA STASHAHADA: MUDA MIAKA 2
UALIMU: MASOMO YA SAYANSI, SAYANSI YA JAMII, BIASHARA NA LUGHA.
- Mwombaji awe mwalimu wa Daraja A aliyethitimu Kidato cha VI na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua “Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja; na awe na uzoefu wa kufanya kazi
kwa muda wa usiopungua miaka miwili (02)

Knowledge’ na ‘Divinity’ hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji, na
UALIMU: ELIMU MAALUM
(i) Mwombaji awe mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na
uzoefu kazini usiopungua miaka miwili (02); na
(ii) Awe mwalimu wa Daraja A aliyethitimu Kidato cha VI na kufaulu kwa kiwango kisichopungua
“Principal Pass” moja na “Subsidiary” moja; na awe na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili (02)

Knowledge’ na ‘Divinity’ hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumudahili mwombaji, na
Mwalimu anayefundisha watoto wenye mahitaji maalum [wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili n.k.
(vithibitisho viambatishwe)], ni sifa ya nyongeza.
3
D: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI NGAZI YA CHETI: MUDA MWAKA 1
UALIMU: SAYANSI KIMU
- Mwombaji awe mwalimu wa Daraja A na awe na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili (02).
UALIMU: ELIMU MAALUM
- Mwombaji awe mwalimu wa Daraja A na awe na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili (02)
- Awe amefaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi: Mwalimu anayefundisha Elimu Maalum hata kama hana mafunzo rasmi ni sifa ya nyongeza
(uthibitisho uambatishwe).
A) VIAMBATISHO
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu watume barua za maombi yao kwa njia ya posta. Barua hiyo iwe na
anuani sahihi ya mwombaji (ya posta, au anuani ya barua pepe), pamoja na viambatisho vifuatavyo
kulingana na aina ya mafunzo:
(i) Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV ,VI na ufundi;
(ii) Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada (kwa waombaji
walioajiriwa); na
(iii)Barua zilizopitishwa na waajiri (kwa waombaji walioajiriwa).
B) MAELEZO MUHIMU
(i) Sifa zilizoelekezwa kwa mafunzo ya ualimu ngazi Cheti Daraja ‘A’ni kwa ajili ya waombaji wa
mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali.
(ii) Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2012 waliojaza nafasi ya mafunzo ya ualimu ngazi Cheti Daraja ‘A’
kwenye “Seforms” wakati wanamalizaelimu ya sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo
kwa njia ya barua na watachaguliwa kwa kufuata vigezo vilivyowekwa.
(iii)Sifa zilizoelekezwa kwa mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wote kwa
vyuo vya ualimu vya Serikali na vyuo vya ualimu visivyo vya Serikali isipokuwa mwombaji kwa vyuo
vya ualimu visivyo vya Serikali anaweza akawa amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2003 na 2013.
(iv)Waombaji wa mafunzo ya ualimu aliyeajiriwa apitishe barua ya maombi kwa mwajiri wake.
(v) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi: www.moe.go.tz, na OWM-TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz;
(vi)Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa Vyuo ambako
watakuwa wamepangwa kupitia anuani zao sahihi.
(vii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM-TAMISEMI:
www.pmoralg.go.tz, kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.
Tanbihi: Kwa waombaji walio Dar es Salaam wanaweza kufika Wizarani na kutumbukiza barua za maombi
kwenye sanduku lililowekwa mapokezi. Tafadhali barua zote za maombi zitumbukizwe kwenye sanduku la
maombi na si vinginevyo.
MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 10 Mei, 2013.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Idara ya Elimu yaUalimu)

CHANZO: http://www.moe.go.tz/
No comments:
Post a Comment