Friday, 14 March 2014

PICHA ZA SALELITE ZA CHINA SI ZA MABAKI YA NDEGE YA MALAYSIA - MAOFISA WA MALAYSIA


Waziri wa ulinzi Hishammuddin Hussein (katikati) akikanusha madai ya ndege kukaa masaa manne hewani kabla ya kupotea.

Picha za satelite za China.
...Askari maji wa singapore wakiendelea kutafuta ndege hiyo wakiwa umbali wa kilometa 700 kazikazini mwa Singapore na kusini mwa china.

...Nchi mbalimbali zinashiriki katika utafutaji wa ndege hiyo zikiwemo meli 42 pamoja na ndege 39.
Kikosi cha Wanajeshi wa hanga wa China wakiendelea kuitafuta ndege ya Malaysia Airlines.
Maafisa wa Serikali ya Malaysia waliokuwa wanadadisi picha zilizopigwa na mtambo wa Satelite wa China ikionyesha kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege iliyotoweka, Jumamosi, wamesema kuwa mabaki hayo yalitoweka na huenda sio mabaki ya ndege hiyo iliyotoweka siku ya jumamosi.

Waziri wa Ulinzi wa Malaysia Hishammuddin Hussein, pia amekanusha madai ya Marekani kwamba ndege hiyo ilipaa kwa masaa mengi kabla ya kutoweka na kupoteza mawasiliano
Amewaambia waandishi wa habari mjini Kuala Lumpar kuwa picha hizo zilizopigwa siku ya Jumapili,saa ishirini na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia kutoweka na abiria 239 zinadaiwa zilitolewa kimakosa na maafisa wa China.
Aidha tetesi kuwa kifaa cha kupeperusha matangazo cha ndege hiyo kimekuwa kikituma taarifa imesemekana kuwa si ukweli .
Waziri huyo amesema kuwa kupotea kwa ndege hiyo sio kitu kilichotararajiwa.
Picha hizo zilitolewa na idara ya serikali ya China ya sayansi na teknolojia siku ya Jumatano.
Bwana Hussein kadhalika amekanusha ripoti ya jarida la Wall Street kwambandege hiyo ilituma data ya Engine yake kwa karibu saa 4 kabla ya kupoteza mawasiliano na kituo cha trafiki ya ndege.
Amesema kuwa juhudi za kuisaka ndege ghiyo zingali zinaendelea.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!