Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila inapofika Machi 8 kila mwaka kwa lengo la kutathmini maisha ya mwanamke na nini cha kufanya ili aweze kuendelea kuyafurahia maisha.
Hii inatokana na ukweli kuwa jamii nyingi zimeshuhudia wanawake wakifanyiwa vitendo vingi vya kikatili vikiwamo kupigwa.
Ili kufanikisha katika hali ya kumletea tija mwanamke wa Tanga, wanawake Wilayani Tanga kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego wameazimia kuiadhimisha kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwamo kufanya mafunzo, kuendesha burudani na kuonyesha kazi zinazofanywa na wanawake wa ukanda huo wa Pwani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Mwanamke Duniani Wilaya ya Tanga, Fortunata Manyeresi anasema watahakikisha wanawake wanaondoka na mambo ya maana katika tukio hilo la Siku ya Wanawake Duniani Tanga.
Anasema jamii inahitaji mbinu za makusudi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowasumbua wananchi nchini.
WANAWAKE WILAYA YA TANGA
Sherehe za mwaka huu zinazobebwa na Kauli mbiu ‘Chochea Mabadiliko Kuleta usawa wa Kijinsia’. Sheria hizo zitafanyika katika Kata ya Usagara, na wananchi wengi wa Tanga wamepania kufanya mambo mbalimbali katika kuadhimisha siku hiyo.
“Tunategemea kuanza shughuli zetu Machi 6. Baadhi ya mambo tutakayofanya ni kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia katika shule mbalimbali za sekondari na msingi za hapa Jijini Tanga. Tatizo la wanawake kufanyiwa ukatili linaendelea kushika kasi Tanga,”anasema Manyeresi.
Aidha mwaka huu, Kamati ya Maandalizi ya sherehe za Siku ya Wanawake Duniani imeazimia kuboresha shughuli za huduma za kifedha (Vicoba) kwa jamii ya watu wa chini na kati kwa kuandaa kongamano kubwa la ujasiriamali na kuwajengea uwezo wanawake.
Mmoja wa wahariri wa Mwananchi,
Dismas Lyassa atengewa banda kwa ajili ya kutoa ushauri kwa watu
Dismas Lyassa atengewa banda kwa ajili ya kutoa ushauri kwa watu
Aidha wanawake hao wa Tanga, wamempendekeza mmoja wa Wahariri wa gazeti hili la Mwananchi, Dismas Lyassa kuwapa ushauri watu kama ambavyo amekuwa akitoa ushauri kupitia vyombo vya habari.
“Lyassa ni kati ya waandishi wa habari ambaye amekuwa kivutio cha wengi Tanga kupitia makala na vitabu vyake, namjua kwa mudfa mrefu, binafsi ni muumini mkubwa makala zake anazoandika kwenye gazeti la Mwananchi kila jumapili na Mwanaspoti kila Jumanne. Hata kabla ya kuhamia katika gazeti hili nilikuwa nasoma sana makala na vitabu vyake vya masuala ya ndoa, saikolojia na ujasiriamali, naamini atasaidia sana kuwaweka sawa watu hapa Tanga”.
Anaongeza kuwa: “Wenye matatizo ya ndoa au uchumba hapa wamefika, ni mtu ambaye anashauri vizuri, hata katika kutathmini, tumegundua kuna wengi ambao wanafuatilia kazi zake hapa Tanga”.

Mambo mengine
MWANANCHI..

No comments:
Post a Comment