Tuesday, 25 February 2014

ANASWA NA KETE 71 ZA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR

Kamanda wa Polisi, Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa

Polisi Kikosi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wamemkamata mkazi wa Temeke, Mwanahamisi Salim (27) kwa tuhuma za kumeza kete 71 za dawa za kulevya aina ya heroini zenye thamani ya zaidi ya Sh60 milioni.
Mkuu wa Upelelezi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Hamad Hamad alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa alasiri ya Februari 20, mwaka huu akijiandaa kupanda Ndege ya Shirika la Emirates kwenda Hong Kong, China.
“Tulipomhoji alitueleza kuwa dawa hizo alikuwa anazipeleka kwa marafiki zake kutoka Nigeria ambao wanaishi Hong Kong lakini bado tunaendelea kumhoji ametoa wapi huo mzigo,” alisema Hamad.
Alisema katika siku za karibuni, wamebaini kuwa watuhumiwa wengi wanaokamatwa ni wanawake.
Alisema wengi wa wanawake hao wanadai wanakwenda kununua vifaa vya saluni.
Kamanda wa Polisi, Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa alisema dawa zilizokamatwa ni heroini.
Taswira ya Tanzania nje
Katika hatua nyingine; taswira ya Tanzania imeendelea kuchafuka baada ya Kituo cha Kimataifa cha Televisheni cha France 24 kutoa ripoti inayoonyesha ukubwa wa tatizo la dawa za kulevya nchini.
Ripoti hiyo inakuja zikiwa zimepita wiki mbili tangu Gazeti la The Mail on Sunday kuandika habari za kukithiri kwa ujangili wa meno ya tembo na pembe za faru.
Taarifa ya kituo hicho ilieleza kuwa Tanzania inaonekana kuwa kituo cha dawa za kulevya kutoka Afghanistan na Pakistan.
Mmoja wa waandishi walioandaa ripoti hiyo, Jaouhar Nadi alisema tatizo la dawa za kulevya Tanzania ni kubwa na hakuna mikakati ya makusudi ya kupambana nalo.
“Zanzibar kwa mfano, kuna watumiaji 10,000 wa dawa za kulevya, yaani katika kila familia moja kuna mteja mmoja. Kuna ‘mateja’ wapatao 250,000 nchi nzima na jitihada za Serikali zinaonekana kuwa dhaifu,” alisema Nadi alipokuwa akihojiwa na France 24 na kuongeza: “Zanzibar kwa mfano, hakuna programu yoyote ya Serikali zaidi ya ile iliyoanzishwa na taasisi ya Kimarekani.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!