Friday, 21 February 2014

UTEKAJI WA NDEGE ETHIOPIA, HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA....

Ndege iliyotekwa ikiwa imetua nchini Uswisi. Picha ya Maktaba

Msaidizi wa rubani wa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, Halimedhin Abera, ndiye aliyebainika kuteka moja ya ndege za shirika hilo hivi karibuni.
Inadaiwa kuwa rubani huyo aliiteka ndege kwa sababu ya kuwa na msongo wa mawazo, baada ya kufiwa na mjomba wake.
Abiria mmoja aliyenusurika katika ajali hiyo anasema, Abera aliwaamuru abiria wote kukaa chini, huku akiwatishia kuzima hewa  ya Oksijeni.

Abera, ambaye amelifanyia kazi shirika hilo kwa miaka mitano, inadaiwa  alifunga mlango wa chumba cha rubani (cockpit) na kubadilisha mwelekeo wa ndege. Awali ndege hiyo ilikuwa ikielekea Italia, lakini akaamua kuipeleka Uswisi aliposema alikwenda kuomba hifadhi. Msimuliaji huyu wa mkasa  anasema baada  ya kuiteka ndege alifungua maski za hewa ya oksijeni na kutishia kuizima kama abiria wasingetulia.
Anasimulia: “Nilifikiri labda kuna tatizo la kiufundi au kwa bahati mbaya mtu amebonyeza sehemu, abiria tulibaki  tukitazamana kwa sura za kuulizana ndani ya ndege.”
Anasema baada  ya muda mfupi, sauti nzito ikizungumza kwa jazba ilisikika kutoka katika vipaza sauti vya ndege ikisema: “Kaa chini, ninazima hewa ya oksijeni”.
Msimuliaji anasema rubani huyo alikaa kimya kwa saa sita bila kuzungumza, huku abiria wakiwa hawajui wanaelekea wapi wala mwisho wao utakuwa vipi.
Anaongeza kusema kuwa  wakati hayo yanaendelea, wahudumu wa ndege waliendelea kugawa vinywaji, huku wakiwatuliza abiria na kuwahakikishia kuwa safari ilikuwa salama.
Hata hivyo, wahudumu hao waliwaambia kuwa, hawana mawasiliano na rubani huyo kwa kuwa ameyakata.
“Wahudumu walikuwa wanagawa vinywaji na kutoa maneno ya faraja, hata hivyo kuna wengine walikuwa wakitokwa machozi mbele yetu,” anasema msimuliaji.
Baada ya kusafiri saa sita kimyakimya, ghafla ndege ilianza kuzunguka huku ikiegemea upande mmoja na baada ya muda ilibadilisha upande wa bawa jingine.
Anasema: “Niliona mwisho wetu umefika kwani ndege sasa inaanguka. Nikitazama nje niliona mwanga lakini baada ya dakika mbili nikaona giza tena,” anasema na kuongeza:
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!