Tuesday 4 February 2014

NYOKA WATIBUA SHUGHURI ZA MAHAKAMA MWANZA.

CHANGAMOTO  nyingi  za  muda mrefu  zinazoikabili  idara ya  mahakama  katika wilaya   ya Ukerewe, Mwanza  sasa zimechukua sura mpya  kwa baadhi ya   shughuri za  mahakama  kuvurugwa  na  Nyoka.



Maelezo  ya  tukio  hilo la aina yake  lililoshutua  wengi  yameelezwa katika    siku ya sheria   ambayo  kiwilaya  ilifanyika  katika  uwanja wa   mahakama ya wilaya  hiyo  mjini  Nansio.

Akizungumzia  changamoto  zinazoikabili  idara  ya mahakama   hakimu  mkazi  wa mahakama ya mwanzo  Bukonyo    Malisel  Ndimila  alisema  hali ya uchakavu  wa majengo  ya mahakama  zote  katika  wilaya hiyo  inatisha.

Akifafanua  alisema  mbali ya changamoto nyingine  ikiwemo  watumishi wa idara hiyo  kutokuwa na nyumba  na  nyezo za  usafiri  lakini  majengo ya  mahakama  hasa jengo la mahakama ya  mwanzo Bukonyo  sasa limegeuka  pango la Popo  na makazi ya  Nyoka.
Katika  maelezo yake   zaidi  Ndimila   alikwenda mbali  zaidi  na kueleza    kuwa tangu  apelekwe  katika mahakama  hiyo hapo mwaka jana  hadi sasa   amenusulika  kuumwa na nyoka  katika matukio  matano tofauti.
Alisema  katika matukio  hayo  Nyoka hao   utokea juu  ya  dali ya  jengo  la  mahakama  hiyo  na  uanguka  chini wakati  mwingine  shughuri za mahakama  zikiendelea  na kusababisha  mtafaluku mkubwa.
Akithibitisha  tatizo hilo  hakimu mkazi  mfawidhi  wa  wilaya  hiyo  Faustin   Kishenyi  alisema  mbali ya  hali mbaya ya uchakavu  wa majengo ya mahakama  pia  watumishi wote  wakiwemo  mahakimu  wote wanne  pamoja na yeye  awana  nyumba.
Nae   Luhasha  Rouben   aliyekuwa  hakimu  wa wilaya  hiyo kabla ya  kustahafu  hapo mwaka  jana   alisema   changamoto hizo  zinatokana  na   idara  hiyo  kutengewa  bajeti  kidogo isiyokidhi maitaji.
Alisema  taarifa zilizopo  zinaonyesha  kuanzia  bajeti  ya miaka  miwili  iliyopita  kuludi nyuma   idara  ya mahakama  kwa nchi  nzima  utengewa  fedha isiyozidi   bil. 17  kwa mwaka  lakini  fedha  inayopelekwa  uwa chini  ya kiasi  kilichotengwa.
Katika  maelezo  yake zaidi  Luhasha   alisema  katika mwaka wa fedha wa  2013/014  idara hiyo  kwa nchi nzima  ilitengewa   sh. Bil 42  lakini  hadi  sasa  fedha  iliyotolewa  ni sh. Bil. 5.5 na  kuzitaka mamlaka za juu  kuwa na  mtizamo mpya  dhidi  ya idara  hiyo vinginevyo  matatizo yataendelea kubaki  kama yalivyo.
Mkuu wa wilaya  hiyo   Mery  Tesha  akizungumza  baada ya kupokea  maelezo hayo  amekili  kuwa  matataizo hayo  yanatokana na ufinyu wa  bajeti  na kutaka wadau  mbali mbali  kushiliki  kutatua .
Hata hivyo alisema  serikali  anatambua  umuimu  wa idara hiyo  na  kuongeza kuwa  wakati  inakamilisha  ujenzi wa  mahakama ya mwanzo  na kituo cha polisi  kwa gharama ya sh. Mil. 250 katika kisiwa  cha Ilugwa pia  imetenga  sh. Mil. 120 kwaajili ya ujenzi wa  mahakama ya mwanzo katika  kisiwa cha  Ukara. Mwisho.
MWANZA  YETU.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!