Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kinatarajia kuanzisha kozi mpya ya mafunzo ya urubani na uhandisi wa ndege, ili kutoa fursa kwa vijana kujifunza fani hiyo ndani ya nchi tofauti na sasa.
Mafunzo hayo yanayotarajiwa kuanza kutolewa Julai mwaka huu, yatafundishwa kwa ufanisi na gharama nafuu lengo likiwa kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao sambamba na nchi kuwa na wataalamu wa kutosha.
Akizungumza wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea chuoni hapo jana, Mkuu wa chuo, Dk Zacharia Mganilwa alisema tayari maandalizi yamefanyika zimebaki hatua za mwisho kuhakikisha wanaanza.
“Tupo kwenye mchakato wa kupata vibali kutokana Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), baada ya wataalamu kuja kukagua kisha tuweke viwango vinavyotakiwa kujifunza kozi hii,” alisema.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alisema ujio wa kozi hiyo utapunguza gharama na nje yanatolewa kwa dola 60,000 za Marekani.
MWANANCHI.













No comments:
Post a Comment