Monday, 10 February 2014

MTOTO WA MGIMWA AIBUKA MSHINDI KURA ZA MAONI KUGOMBEA UBUNGE KALENGA

 Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu Dkt William Mgimwa-picha kutoka maktaba

Mtokeo  ya  kura  za maoni  ndani ya  CCM yametangazwa usiku wa kuamkia leo  huku mtoto wa aliyekuwa mbunge  wa  jimbo hilo Godfrey Mgimwa akishinda kwa  kishindo  katika  nafasi hiyo, akifuatiwa na Jackson Kiswaga katika matokeo hayo.

Godfrey Mgimwa amepata  kura 342 huku Kiswaga  akipata kura 170 na mkuu wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa akiambulia  kura 42 .
  

Matokeo hayo  yaliyotangazwa  katika  ukumbi wa shule ya  sekondari  Mwembetogwa mjini Iringa yanaonesha mgombea Peter Mtisi kapata  kura 33, Msafiri Pangagira kura 8, Bryson Kibasa kura 7, Edward Mtakimwa kura 3 na Thomas Mwiluka akiambulia kura 2

Na Francis Godwin, Iringa

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!