Monday, 10 February 2014

HABARI ZA KIMATAIFA/ WATU 50 WAFARIKI KUTOKANA NA MAFURIKO NCHINI BURUNDI

Kwa mujibu wa waziri wa usalama, mvua kubwa ilinyesha usiku kucha katika mji mkuu Bujumbura na kusababisha uharibifu mkubwa.


Waziri Gabriel Nizigama amesema kuwa tayari wamepata miili ya watu 50, waliofariki baada ya nyumba zao kuporomoka na kusombwa na maji.Majumba yamebomoka kufuatia mvua hiyo kubwa
Mitaa na vitongoji vya mji mkuu Bujumbura viliopo kaskazini vimeathirika zaidi.
Serikali ya Burundi mbali na kutangaza kwamba itagharamia mazishi na huduma kwa majeruhi, imetangaza pia siku moja ya maombolezi ya kitaifa hapo kesho

BBC SWAHILI

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!