Saturday, 22 February 2014

DEREVA WA BODABODA ANYONGWA, MAITI YAKE YATUPWA KATIKA UWANJA WA SHULE KIVULE DAR

Dereva wa Bodaboda aliyejulikana kwa jina la Musa Wambari, 25, mkazi wa Kitunda, jijini Dar es Salaam amekutwa amenyongwa na maiti yake kutupwa katika Uwanja wa Shule ya Abdu Juma huko Kivule.
Marehemu Musa na mkewe enzi za uhai wake.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea Februari 9, mwaka huu saa 4 usiku baada ya marehemu kukodiwa na watu wawili.

Imedaiwa na madereva bodaboda waliokuwa wakiegesha pikipiki zao eneo la Matembele na marehemu kuwa, siku ya tukio wakiwa eneo lao la kazi alifika kijana anayedaiwa kujihusisha na uhalifu aitwaye Jose akiwa na mwenzake aliyevaa suti.
Mmoja wa madereva hao aliyeomba hifadhi ya jina lake aliongeza kuwa, Jose na rafiki yake walitaka kukodi pikipiki lakini kwa vile walikuwa wakimfahamu kwamba alikuwa muhalifu walikataa ndipo wakaondoka.
“Muda mfupi baadaye tulimuona marehemu akiwa anapita na bodaboda yake huku kampakiza Jose na rafiki yake, kwa kuwa hakujua kama hawakuwa watu wema tulijitahidi kumwita ili ahairishe safari lakini kutokana na elementi aliyovaa hakutusikia,” alisema dereva huyo.
Mwendesha bodaboda huyo aliongeza kuwa, walipofika sehemu ambayo ilikuwa imetulia wauaji hao walimuua Wambari kwa kumnyonga kwa mkanda wa suruali aliyovaa kisha kuyatoboa macho yake kwa kutumia wembe na kuutupa mwili wake katika Uwanja wa Shule ya Abdu Juma iliyopo Kivule na kuondoka na pikipiki aliyokuwa akiendesha yenye namba za usajili T538 CSE.
Aliongeza kuwa, mara baada ya kutokea mauaji hayo, Jose alijisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Sitakishari, Ukonga na kudai hakuhusika na mauaji hayo ambapo alishikiliwa hadi alipokuja kutambuliwa na madereva bodaboda na baada ya kubanwa alikiri kumuua Wambari kwa kushirikiana na wenzake wawili kisha kuiuza pikipiki hiyo Manzese ambapo imepatikana.

GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!