Friday 31 January 2014

WAZIRI MKUU WA FINLAND ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM


DSC_0132


Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe(kushoto), akimtabulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka(aliyevaa tai nyekundu) kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen, wakati Waziri Mkuu huyo alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), leo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
DSC_0142Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akitoa ufafanuzi wa namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen(wa tatu kutoka kushoto) , wakati alipotembelea Mamlaka hiyo leo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka. Kulia kwa Waziri Mkuu wa Finland ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na kushoto kwa Waziri Mkuu huyo ni Waziri wa Niashati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.DSC_0151Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Madeni Kipande, akitoa maelezo ya awali ya namna ambavyo Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland,  Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka hiyo leo asubuhi kuangalia namna Mamlaka hiyo inavyofanya kazi. Aidha, Waziri Mkuu huyo alitembelea Gati namba 1-7.DSC_0166Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akichangia mada wakati wa Mkutano na Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) leo asubuhi kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo.DSC_0169Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Finland,  Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo. Nyuma ya Waziri Mwakyembe ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!