Friday 24 January 2014

WAJIPANGA KUPUNGUZA VIFO VYA WANAWAKE NA WATOTO


Mkoa wa Mara umeanza kuchukua hatua mbalimbali za kupambana na ongezeko la vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga.Mkakati huo unaambatana na kuanzisha mpango maalum wa ujenzi wa vituo vya afya ili kusogeza huduma kwa jamii.
Tayari ujenzi wa vituo 12 vya afya umeshakamilika kupitia mpango huo. Hayo yalisemwa juzi katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa huo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Samson Winani, alisema kutokuwepo kwa huduma karibu kuchangia vifo vingi vya wanawake wajawazito na watoto.
Alisema kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo hilo, mkoa umeamua kuboresha vituo vya afya vilivyopo ili sasa vitoe huduma bora
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!